Google tayari wanavunja rekodi katika mafanikio ya kutengeneza maroboti wenye akili sana. Ni hivi karibuni tuu roboti wao alifanikiwa kumshinda mwanadamu katika moja ya mchezo mgumu zaidi duniani wa bao. Swali ni je, hawa roboti hawawezi kututawala siku moja? Mithili ya filamu za Terminator?
Suala hili ndilo lilofanya watu wengine wengi mashuhuri kama vile Stephen Hawking na mmoja wa waanzilishi wa Apple, Steve Wozniak kujitokeza na kupinga juhudi hizi za teknolojia zinazokuwa zina uhuru sana wa kujiamulia na kujiendesha zenyewe. Artificial Intelligence – yaani akili feki, ni uwezo unaopandikizwa juu ya maroboti, kisha roboti hao wataweza kufanya maamuzi mbalimbali wenyewe tena huku wakiwa na asilimia ndogo sana ya kukosea kile wanachotaka kufanya.
‘Project’ ya Google iliyojikita katika teknolojia hii inafahamika kwa jina la DeepMind, nje ya hiyo wanaproject nyingine kubwa ya utengenezaji maroboti janja wanaoweza kutumika jesheni – Boston Dynamics.
Sasa Google wametangaza rasmi ya kwamba kutakuwa na ‘switch’ ya kuzima mfumo wao mzima wa artifical intelligence, hii inawezekana kufanyika pale ambapo roboti husika anaanza kufanya mambo au maamuzi yanayotia wasiwasi.
Suala hili limetangazwa huko nchini Uingereza katika chuo cha Oxford ambapo Google walishirikiana nao katika utafiti wa umuhimu wa kuwa na ‘the red button’ kwa ajili ya kulinda uhai wa binadamu dhidi ya maroboti janja miaka ya baadae.
Je una mtazamo gani juu maendeleo makubwa ya ukuaji wa teknolojia za maroboti? Je unadhani maroboti janja sana ni hatari kwa binadamu hiyo miaka ya baadae?
Chanzo: TechTimes
One Comment
Comments are closed.