Hili limeshawezekana japokuwa bado kuna changamoto za hapa na pale, kwa sasa ni wazi kuwa magemu kutoka huduma ya Google Play Games yanaanza kupatikana kupitia huduma hiyo kwenye kompyuta.
Kwa sasa ni kwa sehemu husika tuu ambapo ndipo unaweza ukawa una uwezo wa kutumia huduma hiyo lakini hapo baadae itawafikiwa watu wengi zaidi.

Kwa sasa huduma iko katika toleo la majaribion, kwa sasa sehemu ambazo zinaweza kupata huduma hii ni Hong Kong, South Korea, Taiwan, Thailand na Australia.
Huduma hii ni mahususi kuwezesha watu kuwa na uwezo wa kucheza magemu ya Android katika kompyuta zao za Windows.
Ukaichana na mengine yote ili kuweza kucheza magemu haya au kufanikiwa kuwa nayo ni lazima kompyuta yake iwe imekidhi vigezo Fulani ambavyo wameviweka.
Vigezo hivyo ni kama. Kompyuta inabidi kuwa na uwezo wa four-core katika CPU, integrated GPU na angalau10GB za ujazo uhifadhi ambazo hazijajazwa katika kompyuta hiyo (Local Disk C).

Uzuri wa huduma hii ni kwamba unaweza ukaanza kucheza michezo hiyo katika kompyuta na kasha kuhamia katika simu yako, na kuanzia pale pale ulipoishia.
Hapana kinachofanyika ni kwamba michezo hiyo inakua na uwezo wa kujihifadhi katika mtandao hivyo kuwezesha kuendelea na pale ulipoishia kwa kutumia ID ya Google.
Kingine cha kukitilia maanani ni kwamba sio michezo yote ambayo ilikua inapatikana kwa vifaa vya Android basi itakua na sifa ya kuja katika kompyuta la-ha-sha.

Hapa ni wazi kabisa kuwa Google ambao ndio wamiliki wa Android wanapambania sana watumiaji wa Windows kuweza kupata michezo hii katika kompyuta zao za Windwos, swali linaweza kuibuka vipi kwa wale ambao sio watumiaji wa Windows?
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment. Je hii umeipokeaje? Je unaweza ukaanza kucheza michezo ya kwenye simu katika kompyuta yako?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.