Google wameleta kipengele kipya kinachoitwa Goals katika app yake ya kalenda wiki hii, Goals inawasaidia watumiaji wa app ya kalenda kuweza kupata muda wa kufanya mambo ambayo wangependa kufanya ila wanakosa muda.
Yapo mambo mengi ambayo mtu unakuwa unania ya kuyafanya lakini swala linakuwa tunakosa muda ama dhamira kuu, unaweza ukawa umejipangia kwamba lazima mwezi huu usome vitabu vitatu kwamfano lakini siku tatu mbele unasahau na ukija kukumbuka siku nyingi zimepita na tayari umekwisha kupoteza muda mwingi.
- Goals inawasaidia watumiaji kukumbuka mambo ambayo katika hali ya kawaida wangeweza kuyasahau, pia kipengele hiki kinaweza kukusaidia kujaribu kutafuta muda katika ratiba zako ili kufanya mambo ambayo umeyaweka katika orodha.
- Goals itakusaidia kuweza kutafuta muda katika ratiba yako na kukukumbusha kufanya jambo ambalo ulipanga kulifanya.
Google wanasema kwamba app hii itazidi kuimarika katika ufanisi iwapo watu wataitumia zaidi na zaidi, ili kutumia kipengere hicho basi mtumiaji anatakiwa kuwa anaweka ratiba ya mambo yake yote katika app hiyo ili iweze kujua wakati hana kazi.
Vyanzo: CTV news na mitandao mingine.