fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google

Gmail Waja Na ‘Smart Reply’ Kwa Ajili Ya Watumiaji Wa Kompyuta!

Gmail  Waja Na ‘Smart Reply’ Kwa Ajili Ya Watumiaji Wa Kompyuta!

Spread the love

Gmail katika kuhakikisha inabaki namba moja, bado inazidi kujiboresha katika huduma zake. Hapa na kipengele chake walichokiboresha, sasa watumiaji wataweza kutuma na kupoke barua pepe kwa urahisi.

kipengele hiki kitakuwa ni kwa ajili ya Inbox tuu na sio Gmail yote kwa ujumla.Inbox ya Gmail ni huduma ya barua pepe katika simu janja na katika kompyuta ambayo  ina toleo lingine la Inbox ambalo limejiboresha katika kuhakikisha watumiaji wake wanapata kilichobora.

Katika Vipengele vipya vilivyoongezwa ni pamoja na ‘Smart Reply’ ambayo kwa mara ya kwanza aliachiwa katika App mwaka jana. Kwa sasa Google imetangaza kuwa kipengele hichi cha ‘Smart Reply’ kimekuja katika Inbox ile ya kwenye Kompyuta.

Muonekano Wa 'Smart Reply'

Muonekano Wa ‘Smart Reply’

Smart Reply bila shaka inasevu muda wa mtumiaji wa huduma hiyo kwa kutoa machaguo matatu ambayo mtumiaji akiyachagua atakuwa amejibu meseji moja kwa moja bila ya kuanza kuandika.  Mtumiaji itambidi achague neno au maneno ambayo anaona yanafaa zaidi katika listi ambayo itatokea wakati akitaka kujibu barua pepe aliyopokea.  Ujumbe atakaochagua itategemea na barua pepe aliyopokea

Vile vile mtumiaji wa huduma hii ana uwezo wa kuhariri ujumbe ambao unaweza ukajitokeza katika ‘Smart Reply’ ili kuboresha jinsi ya kujibu watu wake.

Hii itawasaidia sana watu hasa wale ambao wako bize kama vile wale wa maofisini.  Kwa mfano wale wa maofisini itawabidi wawe wanatumia huduma hii kwani itawasaidia kujipangilia na pia kusevu muda wao.Hebu fikiria kwa kubonyeza sehemu moja tuu unakuwa tayari umeshajibu meseji nzima!. Hili ni la aina yake kutoka Google.Pia Gmail imeongezea kuwa inaweza hata kariri ni jinsi gani mtumiaji anapenda kujibu watu muda kwa muda na kuweka neno/maneno hayo katika ‘Smart Reply’.

SOMA PIA  Apps za Kurekodi Mazungumzo ya Simu, Marufuku kwenye Google Playstore

Google imesema kuwa kipengele hicho kimeshaanza tumika kwa aslimia  10 katika majibu yote ya barua pepe katika Inbox ya simu janja.

Kumbuka pia Google waliachia kipengele chao cha ‘Snooze’ ambacho kinamuwezesha mtumiaji App ya Inbox  kuweza kuchagua ni mda gani ambapo anataka kuiona barua pepe hiyo tena ili aweze kuijibu. Mda huo ulikua ukiuliza “tomorrow,” “later this week,” “this weekend” or “someday.” Yaani “Kesho”, “baadae wiki hii”, “wikiendi hii” au “siku nyingine”. Hapo mtumiaji alitakiwa kuchagua chaguo moja kati ya haya. Pia machaguo haya mtumiaji anaweza akabadilisha tarehe zake.

SOMA PIA  Google: Magari Yetu Ya Kujiendesha Yenyewe Yamepata Ajali Mara 11 Tuu!

Kuweka kipengele cha ‘Smart Reply’ katika kompyuta ni jambo jema sana kwani msaada wake ni mkubwa sana. Niambie wewe umelipokeaje hili. Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari moto moto. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania