Hivi ni mambo mangapi ulitaka kufanya lakini kwa kuwa huna ‘Passport size’ yaka kwama? Ni mengi tuu sio! Sasa vipi kama ungekuwa na uwezo wa kutengeneza picha ya ‘passport size ’ yako mwenyewe ukiwa umetulia nyumbani
Kama unahitaji kwa ajili ya kitambulisho chako au hata kwa ajili ya mambo mengine unajua kabisa ingekuwa ni tabu kidogo. Kwanza ingekubidi uende kwa watu wanaopiga picha hizi na ukimalizana nae inaweza ikakugharimu mpaka Tzs 10,000 kwa picha hiyo.
Unajua ingekuwa rahisi sana na pia usingetumia pesa nyingi kama ungeweza ku ‘print’ picha hizo za uso (passport size) moja kwa moja kutoka katika Pc yako. Lakini hata njia hii pia inakuja na maswali kwa mfano ni saizi gani ya picha hiyo unayotaka? Kwa mfano kwa Tanzania passport size wanazotaka kwa ajili ya kufungulia akaunti katika mabenki na zile katika vitambuliso ni tofauti kabisa. Swali bado linabakia ni saizi gani inayohitajika? Vipi kama wewe ni mkazi wa nchi nyingine hivi watahitaji size gani katika Passport au hata katika nyaraka zingine?
Ukipakua IDPhotoStudio bure kabisa itakuwa ndio suluhisho lako.Mara tuu baada ya kupakua, itafunguka katika kompyuta yako. Kuanzia hapo unaweza anza kuchagua ni picha gani unayotaka kuanza ku’print’
Kinachofuata chagua ni nchi gani na lugha gani ambapo unataka passport size hiyo. Kwa mfano kama ukichagua Us itagundua saizi ya ‘passport size’ na kuipeleka katika vipimo vya Inchi 2 kwa inchi 2. Ukishamaliza sehemu hiyo unaweza ukabofya ‘Print Now’. Au unaweza ukachagua machaguo mengine kama vile kuchagua ni printa gani ya kutumika katika kukamilisha zoezi hilo na pia unaweza ukabdailisha mfumo mzima wa picha. Unaweza ukachagua lugha moja katika ya lugha zaidi ya 30.
Kwa wanotumia Windows wanaweza wakapakua IDPhotoStudio bure Hapa