Mwezi disemba mwaka jana kampuni ya Uber walizindua UberEATS, App ya kampuni ambayo inajitegemea ambayo inahusisha kuwasilisha chakula. App hiyo kwa sasa inapatikana katika soko la iOS na Android.
Uber wamefanya hivyo makusudi, iliwabidi watengeneze App ambayo inajitegemea kabisa kwa kuwa kuomba usafiri na kuagiza chakula ni vitu viwili ambayo haviendani kabisa
Uber ni kampuni kubwa inayojulikana kwa kazi yake kubwa ya kuomba usafiri, yaani kwa kutumia simu yako ndani ya App yao unaweza ukaomba gari ikufuate sehemu na kukupeleka maeneo tofauti tofauti. Kwa mfano mtu unaweza ukaita taxi kwa kutumia App hiyo.
Kitu kama hicho kinaweza fanyika katika App yao ya UberEATS yaani mtu unaweza kutafuta chakula kupita App na kukiagiza.
Kwa sasa App hii inafanya kazi katika maeneo ya San Francisco, Los Angeles, Houston, Chicago na Torronto. Lakini kuna plani kabambe za kuongeza maeoneo mengi zaidi.
Zoezi hili sio gumu kwa Uber wanashirikiana na migawa mingi kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa. Yaani mteja anapoagiza chakula , kwa haraka kinaandaliwa na pia kinapakiwa katika mazingiza ambayo hakitapoa na pia kinakuja kuchukuliwa na mtu atakeyekisafirisha (labda kwa boda boda) mpaka kwa mtu aliyeagiza (mteja). Mteja ataweza pokea chakula chake baada ya dakika chache tuu kwani kwa kule migahawa iko mingi sana.
“Ukiwa tayari kuweka oda ya chakula chako utaonaona kabisa bei imewekwa hapo, Unaweza kulipia chakula hicho kwa kutumia akaunti yako ya Uber na usubiria msosi wako ukikufikia kwa kutumia App” – walisema UberEATS.
Gharama ya usafirishaji itakua ni kati ya dola 8 mpaka 12 za marekani (Tsh 17 mpka 25 kwa haraka haraka)
UberEATS imeingia katika ushirikiano na migahawa kama Dinosaur BBQ, Dimes Deli, Tiny’s Giant Sandwich Shop na The Brindle Room nab ado wana mpango wa kuongeza namba hii. Watu wenye migahawa mbalimbali wanashauriwa kujiunga katika mkakati huu kwa kujiunga kupitia tovuti yao ambapo itawbidi wajaze fomu.
Huduma ya usafiri ya UBER ipo njiani kuanza kupatikana Tanzania hivi karibuni.
UberEATS inarahisisha ile hali ya kutoka A kwenda B ili tuu kupata chakula. Kumbuka unaweza kaa na ukatumia App yako na ukapata msosi, safi kabisa..!