fbpx
Teknolojia

OS Fuchsia Inaweza Kuwa Mbadala Wa Android Kutoka Google!

fuchsia-ni-mbadala-wa-android
Sambaza

Sio siri kuwa kampuni ya Google ilikua na mpango wa kutengenezea mfumo endeshaji ambao ni mbadala kwa Android. Ikumbukwe kuwa Android ndio mfumo wa uendeshaji ambao umezoeleka sana na umesambaa katika simu nyingi duniani  kuliko mwingine wowote.

Jambo hili halikua siri sana kwani hata jina lako OS hiyo limewekwa wazi kuwa itaitwa Fuchsia ripoti zinasema kuwa Google wamekua wakiwa wakilifanya swala hili kwa kipindi cha muda mrefu tuu lakini hakukuwa na vithibitisho thabiti.

INAYOHUSIANA  Dondoo kuhusu Samsung Galaxy Note 10 Pro

Mpaka sasa ni kwamba Kampuni imeweka katika mtandao baadhi ya taarifa za OS ya Fuchsia na pia wale wakosoaji na waboreshaji (developers) wamepewa uwezo wa kuweza kutumia Os hiyo na kutoa maoni yao katika mtandao.

Screenshot Ya OS Fuchsia Kutoka Google
Screenshot Ya OS Fuchsia Kutoka Google

Ma’developer wote wanaweza fuatilia OS hii kwa kuingia katika mtandao spesho unaujulikana kama Fuchsia.dev ili kuweza kuwasilisha mawazo yao kuhusiana na OS hiyo.

Ukiingia katika mtandao huo kuna taarifa mbalimbali na nyaraka ambazo zinahusu OS Fuchsia na pia mtandao huu utakuwa ni wa wazi kama vile ilivyo kwa upande wa Android. 

INAYOHUSIANA  Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona

Fuchsia itakua inapatikani katika vifaa vyote– kuanzia simu janja mpka kompyuta– Os hii, tangia mwishoni mwa mwaka 2016 imekua katika hatua za mwanzo mwanzo tena kwa siri lakini kwa sasa mambo yamebadilika na iko wazi katika macho ya watu.

Soma Zaidi Hapa Kuhusu Fuchsia

Je unadhani teknolojia ya OS hii itapata umaarufu zaidi ya ile ya Android? ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya maoni.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Sayansi Na Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com