fbpx

Facebook

Facebook Na Ununuzi GIPHY, Nini Tutegemee!

facebook-yainunua-giphy

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Facebook imenunua kampuni maarufu ya kutengeneza picha zinazojongea maarufu kama GIF. Kampuni hiyo inakwenda kwa jina la Giphy.

Ni wazi kuwa Giphy ni kampuni ambayo imejikita tuu katika picha mjongea, FB imenunua kampuni hiyo lakini taarifa nzima za dili hilo halikuwekwa wazi, japokuwa kuna vianzo vingine vimesema kuwa ni takribani dola mia 4 za kimarekani.

Giphy
Giphy

Kumbuka Giphy ni kama mtandao wa kijamii tuu ambao unatumika ku’share’ picha jongefu kwa ndugu, jamaaa na marafiki.

INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya Facebook kuwa salama kwa kuondoa programu usizozihitaji

Kwa mujibu wa Facebook, lengo la kuinunua kampuni hiyo ni kuiunganisha na kampuni yao ya Insatgram. Kwa mantiki hiyo ni kwamba tarajia kuona GIF kama kipengele ndani ya mtandao wa Instagram ndani ya siku zijazo.

Ukiachana na hayo FB wameweka wazi kuwa kampuni ya Giphy itakuwa inajitegemea kwa kufanya kazi nje ya vipengele vya Facebook. Vile FB imewaka wazi kuwa watu wengi wanautumia Giphy huwa watoka katika mtandao ya kijamii ya Instagram, Facebook, Messenger na WhatsApp na mara nyingi huwa wana’share’ GIF hizo katika mitandao hiyo.

INAYOHUSIANA  Kuna uwezekano wa WhatsApp Na Facebook Kuunganishwa, Nini Nyuma Ya Pazia?

Niambie wewe unahisi baada ya kampuni hii kununuliwa Facebook itabadilika katika nyanja gani? niandikie hapo chini katika eneo la maoni. Pia kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com