fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti

Facebook Waruhusu Matumizi ya Video Fupi Kama Picha ya Profile

Facebook Waruhusu Matumizi ya Video Fupi Kama Picha ya Profile

Spread the love

Mtandao wa jamii mkubwa duniani wa Facebook umekuja na mambo mapya katika kuboresha zaidi mtandao huo. Kipya katika mtandao huo itakuwa uwezo wa watumiaji kuweza kuweka picha ambazo ni video fupi za takribani sekunde 7 zitakazoweza kujicheza mara moja mtu anapokuwa katika eneo linaloonesha picha ya ‘Profile’ ya mtumiaji.

'Profile Picture' itakuwa inaonekana kwenye eneo la kati kwenye simu. Pia utaweza pia kuchagua mambo spesheli kama vile picha uzipendazo kuwa kwenye utambulisho wa kwenye habari zinazokuhusu kwenye Profile yako

‘Profile Picture’ itakuwa inaonekana kwenye eneo la kati kwenye simu. Pia utaweza pia kuchagua mambo spesheli kama vile picha uzipendazo kuwa kwenye utambulisho wa kwenye habari zinazokuhusu kwenye Profile yako

Mtandao wa Facebook unawatumiaji zaidi ya bilioni 1.49 duniani kote, uwezo huu wa kuweza kutumia video fupi kama ‘profile picture’ umeanza kusambaa taratibu kwa watumiaji wachache kwa majaribio na utaendelea kusambaa kwa wengine wote.

SOMA PIA  TTCL Kuongeza Uwezo wa Mawasiliano ya Simu maradufu!

Mabadiliko haya yanafanyika kwa ajili ya kuzidi kupendezesha mtandao huo kwa watumiaji wa simu za mkononi. Vingine vipya itakuwa ni pamoja na mabadiliko ya eneo la ‘profile picture’, litasogezwa kwenda katikati ya eneo la ‘coverphoto’.

Pia profile picha zitakuwa kubwa zaidi kulinganisha na muonekano wa sasa

Pia kingine kipya ni pamoja na uwezo wa mtumiaji wa mtandao huo kuchagua picha kadhaa azipendazo kuwa picha kuu za kwanza kuonekana katika eneo la profile yake.

Uwezo wa kuweka 'profile picture' ambazo zitatoka mara moja baada ya muda uliouweka

Uwezo wa kuweka ‘profile picture’ ambazo zitatoka mara moja baada ya muda uliouweka

Utaweza pia kuwa na picha za Profile za muda mfupi, yaani utaweka ‘profile picture’ ambayo utaipa muda wa kutoka (ku’expire). Picha hiyo itabadilika mara moja baada ya muda wake uliouchagua kuisha.

SOMA PIA  Firefox Sasa Kupatikana Apple store Kwa Watumiaji wa iPad na iPhone

Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Facebook unajitahidi kufanya mabadiliko makubwa ili kuzidi kuwavutia watumiaji wa mtandao huo kutumia muda mwingi zaidi katika mtandao huo.

Je umevutiwa na mabadiliko haya?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania