fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Apple Facebook Intaneti

Apple dhidi ya Facebook – Mapato ya biashara ya Matangazo Facebook hatarini. #Data #Usalama

Apple dhidi ya Facebook – Mapato ya biashara ya Matangazo Facebook hatarini. #Data #Usalama

tecno

Kuna ugomvi mkubwa kwa sasa kati ya Apple dhidi ya Facebook kwenye masuala ya usalama wa data za watumiaji simu. Kampuni ya Apple imesema inafanyia kazi kuwezesha watumiaji wa simu na tableti zake kuwa na uwezo wa kuchagua kutoruhusu apps kama za Facebook kufuatilia utumiaji wao wa simu na data zao zingine binafsi zinazotumiwa na Facebook kwa ajili ya biashara ya matangazo.

Facebook wakiongozwa na Mark Zuckerberg wamekuwa wakirudisha shutuma kwa Apple kwa maamuzi hayo wakisema suala la utumiaji data katika matangazo ni kwa ajili ya kuhakikisha watumiaji wao wanapata matangazo yaliyo sahihi.

apple dhidi ya facebook

Mabadiliko hayo yanakuja kwenye programu endeshaji ya iOS 14

Fahamu jinsi Facebook inavyofanya biashara

Unapopakua app yeyote ya Facebook kama vile Facebook yenyewe, Instagram au WhatsApp, muda wote kuna data kuhusu simu yako, mtandao, eneo ulilopo huwa zinatumwa kwenda Facebook. Pia je kuna apps zingine ambazo umelogin kwa kutumia Facebook? Basi Facebook anapata kufahamu hivyo pia. Kwa kufahamu maeneo unayotembelea na vitu unavyofuatilia kwenye apps za Instagram na Facebook mfumo wa kompyuta unaweza kufahamu wewe ni mtu wa aina gani.

Kupitia data hizi mfanyabiashara anaye nunua matangazo ya Facebook au Instagram anaweza kutangaza akilenga aina flani ya watu – mfano wanaopenda mpira, au wanaopenda kwenda kwenye migahawa… au watumiaji wa simu za aina flani. Pia ata anaweza kuhakikisha tangazo lake linaonekana kwa watu wanaoishi maeneo flani tuu – mfano Ubungo tuu, au Dodoma tuu.

SOMA PIA  Apple Watch yasaidia kuokoa maisha ya binadamu

Ili kufanikisha uwezo wote huo mfumo wa biashara ya matangazo ya Facebook unategemea data za watumiaji wa mtandao huu wa kijamii.

Mabadiliko ambayo Apple anayaleta

Apple atawawezesha watumiaji wake kuchagua ni vitu gani wanaruhusu app kufuatilia. Utapewa uwezo wa kuwasha na kuzima vitu unavyoruhusu pale unapoanza kuinstall/kupakua app yeyote. Kwa kufanya hivi Facebook wanaamini watumiaji wengi watawanyima uwezo wa wao kuwafuatilia na utumiaji wa data zingine zinazo wahusu.

apple dhidi ya facebook

Apple dhidi ya Facebook – Watumiaji wataweza kukubali au kukataa kuruhusu app kutumia data zake.

apple dhidi ya facebook

Mkurugenzi wa Facebook amefanya juhudi kubwa za kutafuta kuungwa mkono kupinga maamuzi ya Apple

Mkurugenzi wa Facebook, Bwana Mark ameanzisha kampeni kubwa dhidi ya maamuzi ya Apple. Kampuni ya Facebook imenunua matangazo katika magazeti makubwa nchini Marekani kama vile The Wall Street Journal, New York Times, na Washington Post ikiomba watu wengi wajitokeze kupinga uamuzi wa Apple. Facebook wanashtumu Apple kwa kufanya maamuzi yenye athari kubwa dhidi ya biashara kubwa na ndogo ambazo zinategemea mfumo wa matangazo ya Facebook katika kujiendesha na kutoa ajira. Apple wamejibu shutuma hizo wakisema Facebook hawaheshimu utumiaji wa data za watumiaji wake na ni muhimu watu wawe na haki ya kukubali au kukataa suala la data zao kutumiwa na Facebook kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe kibiashara.

SOMA PIA  App Store: Apple waiondoa app ya Telegram kwenye soko lake la Apps

Vipi una mtazamo gani juu ya jambo hili? Watafiti wanaamini uwezo huo utakapoanza kupatikana kwenye simu za iPhone basi Facebook wanaweza poteza asilimia 10 au zaidi ya mapato yao ya biashara ya matangazo. Pia kuna wasiwasi kama jambo likipendwa na wengi basi tusishangae likasambaa hadi kwa simu za Android pia.

Vyanzo: Facebook, The Verge na vingine mbalimbali

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania