fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Facebook Inacheza na Uwezekano wa Kusafirisha Fikra.

Facebook Inacheza na Uwezekano wa Kusafirisha Fikra.

Spread the love

Wangapi kati yetu tunafikiria kwamba kuna siku itafika tutaweza kukutana na watu popote duniani bila kutumia usafiri? Mbali na kuonana na kusikiana, kitu ambacho tayari kinafanyika kirahisi, facebook wanafikiria kuleta uwezo wa kukutana katika chumba kimoja – kidijitali na hii ndiyo ‘virtual reality’.

Kampuni ya Mark Zuckerberg, Facebook inatazamia kutumia teknolojia ya Oculus Rift, walionunua kwa takribani dola bilioni 2 za kimarekani kuweza kusafirisha fikra na kuwapa watu hisia ya kuonana popote duniani. Hili limesemwa na Mike Schroepfer, afisa mkuu wa teknolojia (CTO) wa kampuni ya Facebook wakati wa mahojiano na waandishi wa habari kabla ya Dublin Web Summit iliyofanyika hivi karibuni.

Oculus inatumia vifaa maalumu vya kuona na kushiriki kwenye dunia ya kusadikika

Oculus inatumia vifaa maalumu vya kuona na kushiriki kwenye dunia ya kusadikika

Jambo hili halitakuwa kazi rahisi kwani changamoto kubwa iliyokuwepo ni kuzifanya hisia za mwili kuamini kwamba kweli mwili upo mahala fulani na siyo ulimwengu wa kusadikika. Kutembea, kupata mrejesho wa papo kwa hapo na kushirikisha mambo ya ukweli yanayotokea kwenye dunia ya kweli ni baadhi ya changamoto ambazo pia si rahisi kuzikabili ila kwa kutumia “controller” za Oculus Rift zinazotarajiwa kupatikana kuanzia mwaka ujao, facebook itapunguza changamoto hizi.

Baadhi ya "controller" za Oculus Rift

Baadhi ya “controller” za Oculus Rift

Katika harakati nyingine, Facebook wanashirikiana na makampuni ya filamu kutengeneza dunia ya kuaminika kwa ajili ya Oculus Rift. Kampuni ya Surreal Vision pia imenunuliwa na kuanza kufanya kazi na Oculus Rift kwa ajili ya shughuli hii na inaripotiwa kwamba maendeleo yake ni ya kustaajabisha.

SOMA PIA  Muundo mpya wa roketi iliyotengenzwa SpaceX

Wakati tukitegemea maajabu haya ya kuweza kutumia teknolojia ya kuwepo popote duniani ndani ya miongo michache baadae, Facebook kwa sasa wanaitumia Oculus Rift kwenye soko la magemu.

Tazama video fupi kuhusu Oculus Rift kwa lugha ya kiingereza hapa chini.

Picha Na: Digitaltrends, tweakTown, Metro – UK

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Comments

  1. […] post Facebook Inacheza na Uwezekano wa Kusafirisha Fikra. appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania