fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps

Brilliant: App Itakayo Kujulisha Kuwa Una Upeo Kiasi Gani!

Brilliant: App Itakayo Kujulisha Kuwa Una Upeo Kiasi Gani!

Spread the love

App zinazuhusisha michezo ya kuuliza maswali ya kusisimua lakini yanayohusisha ukweli almaarufu kama ‘Trivia’ ni mizuri. Lakini kwa muda mwingine yanakuwa na maswali ya ajabu ajabu ambayo mara nyingine yanabeba taarifa zisizo na maana kwa mfano unaweza ulizwa swali kama ‘waandishi wa teknokona huwa wanakula chakula gani?”.

Ndio, unaweza ulizwa swali kama hilo, lakini nafikiri hakuna mtu anaejali hayo. Kama unataka kujibu maswali magumu zaidi na yenye changamoto za kutiisha basi huna budi kuijaribu App ya Brilliant. App ambayo inakupa maelfu ya maswali katika ulimwengu wa sayansi, hesebu na mantiki yote hayo kwa ajili yako. Licha ya kupewa taarifa ambazo hazina maana kutoka katika michezo mbalimbali ya Trivia, utakuwa unaiweka akili yako katika hali (afya) nzuri na hata uwezo wa kufikiria utaongezeka.

SOMA PIA  Sasa Unaweza Kuona SMS Zako Zote za kwenye simu kupitia Pushbullet

Ngoja Nikupe Mfano Ujionee Aina Ya Maswali Yanayoulizwa

brilliant

Baada ya kudhani unalijua jibu bofya “Check answer.” ili kuangalia kama umepatia au umekosea na pia unaweza bofya “view solution” ili kuona njia.

Unavyozidi kujibu maswali ndivyo unavozidi kupanda chati/ngazi. Pia uunaweza kujiunganisha na wenzio ambao wanatumia App hii ya Brilliant na kuanza kushindana

MUHIMU: Ukijiunga kutumia app ya Brilliant, utapokea barua pepe nyingi sana na mara nyingine inakuwa hadi zaidi ya moja kwa siku. Lakini hili sio tatizo kwani utakuwa na uwezo wa kujiondoa katika orodha ya wale wanaozipata barua pepe hizo (za kukera) kwa kujiondoa yaani ‘ unsubscribe’

brilliant

Brilliant – iOsShusha

Brilliant – AndroidShusha

Nina imani kuwa tukipunguza kucheza magemu mengine katika simu ambayo hayana maana na kuanza kutumia App kama hii (Brilliant) katika kuweka vichwa vyetu sawa itatusaidia sana.

SOMA PIA  Kenya nayo yafikiria kudhibiti WhatsApp na Skype

Noa akili yako na App hii ya Brilliant. Cha muhimu ni kwamba App hii haina umri hivyo kila mtu anaweza tumia. Tuandikie sehemu ya comment juu ya mapokezi yako kwa App hii. Tembelea TeknoKona Kila Siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] post Brilliant: App Itakayo Kujulisha Kuwa Una Upeo Kiasi Gani! appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania