fbpx
apps, Intaneti

Huduma ya Mawasiliano ya Zoom yakosekana kwa Wengi

mawasiliano-ya-zoom-yakosekana-kwa-wengi
Sambaza

Huduma maarufu ya mawasiliano ya Zoom yakosekana kwa wengi duniani kote kwa masaa mengi katika tukio linalohusishwa na tatizo la kiufundi.

Huduma ya mikutano kwa njia ya mitandao kupitia video ya Zoom imepata umaarufu na kukua kwa haraka baada ya ujio wa Corona /covid19.

Huduma hiyo inategemewa na maelfu ya watu na makampuni katika kuwezesha mawasiliano na vikao vya kila siku kwa njia ya mtandao.

INAYOHUSIANA  Google kukuambia kama password yako imedukuliwa! #Extensions

Upotefu wa huduma hiyo umetokea karibia katika bara yote duniani wateja wa Marekani, Ulaya na ata Afrika Kusini wakiathirika zaidi. Wateja wengi walienda kulalamika mitandaoni hasa hasa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuonesha kutofurahishwa kwao.

Huduma zilizoathirika zaidi ni huduma za vikao vinavyohusisha watu wengi – Zoom Meetings na Zoom Webinars. Huduma zingine kama vile Chat zimeendelea kufanya kazi.

INAYOHUSIANA  Mchezo wa kushinda kiurahisi

Baada ya masaa mengi ya kufanyia kazi jambo hilo Zoom wamesema tayari huduma hiyo inatakiwa imeanza kurudi kwenye ufanisi kwa watumiaji wake wote.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*