Kampuni ya Smile Communications ambao wanaongoza kwa kutoa huduma ya kipekee ya intaneti ya 4G katika nchi mbalimbali barani Afrika (Tanzania ikiwemo), wamelipatia shirika la Ericsson mkataba mnono wa kusimamia mitambo yake katika nchi zote ambazo Smile inafanya kazi.
Katika mkataba huo kampuni ya Ericsson itahusika na kusimamia mitambo ya kampuni ya Smile na pia kusaidia kampuni hiyo katika matengenezo na uwekaji wa mitambo/teknolojia mpya katika maeneo yote ambayo Smile inatoa huduma zake.
Kwa takribani miaka 15 kampuni ya Ericsson imekuwa inalipwa na mashirika mengi ya simu katika kutengeneza, kuweka na kusimamia mitambo ya miwasiliano katika nchi za Afrika Mashariki
Hii ni mara ya kwanza kwa Smile kuamua kuacha kazi hiyo kusimamiwa na kampuni moja katika nchi zote ilizopo, kampuni kampuni ya Ericsson ilikuwa na mkataba kama huo nchini Nigeria tu na walikuwa na mikataba kama hiyo na makampuni mengine tofauti katika nchi zingine.
Kampuni ya Ericsson ndiyo moja ya makampuni makubwa kabisa katika teknolojia ya mawasiliano na huwa inapata mikataba kama hii katika nchi nyingi duniani kote.
Katika suala la teknolojia ya 4G/LTE mitambo iliyochini ya kampuni ya Ericsson inasaidia zaidi ya watu bilioni 1 duniani kote kupata huduma hii kupitia mikataba kama hii na Smile. Pia inasemekana takribani asilimia 40% ya data nzima za mawasiliano zinazotumika kila siku huwa zinapitia katika mitandao inayosimamiwa na kampuni ya Ericsson. Mkataba na Smile Communications ni wa miaka mitano.
No Comment! Be the first one.