Mtandao wa barua pepe unaomilikiwa na kampuni ya Google wa Gmail umeleta rasmi uwezo wa mtu kurudisha barua pepe ambayo alikwisha bofya alama ya kuiruhusu kwenda, yaani ‘Send’.
Uwezo huu ulikuwepo kwa miaka kadhaa kwa watu wachache ambao iliwabidi wapitie eneo la Google Labs kuweza kuuwezesha.
Kama utakuwa umekosea barua pepe ya kwenda kwa rafiki ukamtumia bosi wako n.k basi uwezo huu utaweza kukusaidia sana kuepuka majanga ya namna hii.
Kuwezesha chaguo (setting) hii ingia kwenye mtandao wa Gmail na kisha nenda eneo la ‘Setting’ la barua pepe yako.

Bofya tiki eneo la ‘Enable Undo Send’ kisha chagua muda wa kuchelewa kwa ujumbe kutumw (muda upo ktk sekunde).

No Comment! Be the first one.