Android inaleta sasisho (update) katika programu endeshaji (OS) yake ambayo pamoja na mambo mengine itakuja na seti mpya ya emoji. Watumiaji wa simu za Nexus ndio watakaoanza kupata hizi Emoji hizo wiki ijayo na kwa watumiaji wengine itabidi kusubiri mpaka pale ambapo watengenezaji wa simu zao watakapokuwa tayari kuwapa update hiyo.
Mkuu wa Android Hiroshi Lockheimer amesema kwamba emoji hizi mpya sasa zitapatikana kwa watumiaji wa Nexus kuanzia wiki ijayo(baada ya kupata update) na baadaye kwa watumiaji wote wa Android(ambapo watumiaji wengine itategemea na watengenezaji wa simu husika lini watatoa hizo updates kwa simu zao),emoji mpya hizi ni zile za Unicode version 8 ambazo zinahusisha emoji mpya 37.
Mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja watumiaji wa iOS walianza kutumia iOS 9.1 ambayo pamoja na mambo mengi ilikua na seti ya emoji mpya,hii iliwapa watumiaji wa vifaa vya Apple kitu ambacho watumiaji wa android hawana. Kwa kipindi hicho chote watumiji wa Android wamekuwa wakizikosa emoji hizi mpya.
Mabadiliko haya yatakuja na keybord fonti na code mpya hivyo inaonesha mabadiliko ya makubwa ya OS hayatakwepeka, ingawa bado haijajulikana hasa mabadiliko mengine ambayo yatakuja na pamoja na mabadiliko hayo lakini ni wazi kwamba kuna mengi yatabadilika.
Je ulichoshwa na watumiaji wa iPhone kukuzodoa juu ya emoji mpya? pengine hii itasimama kwa muda pindi simu yako ya Android itakapo pata update hii, ingawa kwa wakati huo pengine iPhone itakuwa ishaleta kitu kingine maana toleo jingine la emoji linatarajiwa kutoka katikati ya mwaka 2016.
Endelea kufuatilia Teknokona katika mitandao ya kijamii kwa ajiri ya kupata taarifa zinazotoke kwa wakati, tufuate katika mitandao ya Twitter Facebook na Instagram kila unapokuwa na chochote usisite kutushirikisha.
One Comment