fbpx

WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Utakumbuka miezi kadhaa tulishawahi kuandika kuhusu kuweza kupiga simu za sauti/video kwenye WhatsApp, sasa hilo limetimima kwani kipengele cha kupiga simu kwa njia ya sauti au video kimewekwa katika makundi (WhatsApp Group).

Ingawa WhatsApp wenyewe hawajathibitisha rasmi kipengele hicho lakini tayari kinapatikana katika toleo la WhatsApp Beta. Mwezi uliopita katika mkutano wa F8 Facebook ilithibitisha ujio wa kipengele hicho mwishoni mwa mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Samsung yawaomba watumiaji wa Galaxy Note 7 kuacha mara moja

Kwa kuwepo kipengele hicho kuanza kupatikana katika toleo la WhatsApp Beta ni kiashirio kwamba wakati wowote watumiaji wa WhatsApp wataanza kupata sasisho hilo.

Kawaida kipengele kipya (sasisho) chochote huanza WhatsApp Beta kama sehemu ya majaribio na kisha hufuatia watumiaji wake wa kawaida. Kwa sasa kitu hicho kinapatikana katika toleo la WhatsApp beta la 2.18.189 na v2.18.192.

kwa njia ya sauti

Kwenye mkutano wa F8 Mwanzilishi wa Facebook ndio aliweka wazi kuwa kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi ya WhatsApp ni kitu ambacho kipo mbioni kuja.

Namna ya kupiga simu kwenye kundi ni kama hatua za kumpigia mtu mwingine yeyote kwenye WhatsApp, lakini hii ya kwenye kundi kutatokea kipengele cha ‘Add Participant‘ ambapo muhusika atabonyeza na atakuwa amewaunganisha washiriki wote kwenye kundi, au yule atakayepokea simu hiyo kwenye kundi pia atakuwa anaweza kuongeza washiriki wengine kwenye kundi.

Ujio wa kipengele hiki utasaidia sana wanakundi kufanya mijadala kwa njia ya sauti hata video kulingana na mahitaji yao na kupunguza kutuma ujumbe ambao wakati mwingine huleta usumbufu kwa wanakundi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.