Mwisho wa mwaka na tunajaribu kuangalia vitu mbalimbali vilivyobamba zaidi kwa mwaka huu, hapa tutaangalia kwa upande wa emoji kumi ambazo ndio zimebamba zaidi mwaka huu.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizo kusanywa kutoka kwa watumiaji wa keyboard za emoji zinazotengenezwa na kampuni ya Apalon Apps.
Apalon ni moja ya kampuni inayoheshimika zaidi katika utengenezaji wa apps mbalimbali zinazofanya vizuri kwenye masoko ya apps ya Apple Store, Google Play na Amazon.
-
Uso wenye machozi ya furaha.
Hii ni emoji ambayo wengi wetu huitumia kuonesha furaha iliyo pita kiasi, binafsi hii huitumia kuonesha kwamba nimechekeshwa sana juu ya jambo fulani. Hii ndio emoji bora zaidi kwa mwaka 2015 kama wewe unaipenda basi naomba nikuambie kuwa haupo peke yako.
2. Uso wenye furaha na macho yenye umbo la kopa.
Wengi hutumia emoji hii kuonesha kupenda ama kutamani kitu, maranyingi katika picha za kuvutia za watu vyakula ama vitu. Emoji hii imepewa namba mbili katika emoji kumi bora za mwaka 2015.
3. Dole Gumba.
Alama ya dole gumba likiangalia juu alama tunayo itumia zaidi kusema ndio ama poa ndiyo emoji iliyoshika namba tatu katika chati hii. Pengine uchaguzi wa mwaka huu pia ulichangia kuipa emoji hii chati maana ndiyo ilikua inatumiwa na washabiki wa chama tawala kilichoshinda uchaguzi mkuu hapa nyumbani Tanzania.
4. Uso ukiwa umetoa macho na ulimi uliotolewa nje.
Hii emoji huwa kwangu huwa inatumika kushushua watu ama pia kuonesha kuwa nimeaibika, sijui wewe msomaji unaitumiaje hii emoji lakini jambo la msingi ni kwamba hii ndiyo emoji ambayo imeshika namba 4 katika emoji kumi za mwaka huu.
5. Makofi.
Hii ndiyo alama namba tano kwa ubora kwa mwaka huu wa 2015, ni alama tunayotumia kupongeza na maranyingi inatumika pindi tunataka kupongeza kitu ama mtu juu ya jambo fulani.
6. Emoji ya kukenua.
Hii ni emoji ambayo ilianza kutumika mwaka 2010 katika unicode toleo la 6, inatumiwa zaidi pindi mtu napokuwa amefurahia jambo ama anachekelea jambo kwa kukenua meno.
7. Emoji ya Kubusu
Emoji hii inatumiwa zaidi katika mahaba ingawa pia wapo wanaoitumia kuonesha kuwa wamekipenda kitu au mtu. Hii emoji imeshika namba 7 katika emoji bora zaidi za mwaka 2015, ingawa wapo wengi ambao wanaitumia hii emoji kuliko nyingine zilizotangulia lakini kwa mujibu wa Apalon hii emoji ipo namba saba.
8. Busu.
Emoji hii inayoonesha alama ya busu la mwanamke, ni kama alama inayobaki sehemu iliyobusiwa na mdomo. Kwa mwaka huu hii emoji imeshika namba nane kwa mujibu wa kampuni iliyofanya utafiti huo.
9. Uso watabasamu na mdomo wazi.
Hii ni emoji ya uso uliotabasamu huku mdomo ukiwa wazi na meno yakionekana kwa kiasi, mimi naitumia zaidi emoji hii nikiwa nacheka na naamini wengi hamtofautiani na mimi. Emoji hii imesimama katika namba tisa ya msimamo huu.
10. Emoji ya Simanzi/Fikra nzito.
Emoji hii ndiyo iliyoshika mkia katika emoji za mwaka 2015, wengi huwa tunatumia emoji hii kuonesha simanzi juu ya jambo fulani lakini ukweli ni kwamba emoji hii ilibuniwa ili kuonesha mtu akiwa katika mawazo ama katika hali ya fikira zaidi.
No Comment! Be the first one.