wafanyakazi wengi wanazidi kufyeka katika makampuni yanayojihusisha na teknolojia, hivi katiruni tuliandika kuhusiana na Meta na sasa ni zamu ya Disney.
Ni wazi kwamba Disney ni moja kati ya makampuni makubwa sana duniani na inajihusisha na mambo kadha wa kadha ikiwemo teknolojia.
Kwa sasa habari hii ya kupunguza wafanyakazi bado haiko rasmi sana maana kwa taarifa za chini chini ni kwamba habari hii imevuja kabla ya tangazo rasmi kutoka katika kampuni.
Lakini kwa viashiria vyote vinaonyesha kuwa jambo hili linaenda kutokea kwa siku za hivi usoni ili kuhakikisha kuwa inapunguza gharama za uendeshaji.
Ukiachana na kupunguza tuu wafanyakazi kampuni inasadikiwa hata kupunguza au kuachana kabisa na swala zima la uajiri wa wafanyakazi wapya.
Hili ni jambo bay asana kwa kampuni yoyote ile lakini kingine ni kwamba kama watalazimika kuajiri watu wapya basi itakua ni katika yale maeneo ya msingi na ya muhimu sana.
Disney sio kampuni ya kwanza kufanya haya kumbuka makampuni kama vile Warner Bros Television, HBO Max na Netflix na wenyewe wamepunguza wafanyakaza kwa kiasi kikubwa tuu.
Kwa Disney mpaka sasa haijajulikana juu ya ni wafanyakazi wangapi ambao watapunguzwa. Moja ya njia ambayo wataitumia katika kuhakikisha wanapunguza gharama ni kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.
Disney hata wao wamekua wakishangaa maana waliongeza hata bei katika vifurushi vyake lakini bado mapato sio mazuri kama ilivyotegemewa.
Niandikie hapo chini katika eneo la comment, unadhani kampuni ifanye kitu gani katika kuhakikisha kuwa inazidi kupata mapato manono? Je kupunguza watu kazi ni njia sahihi ya kuepukana na hili?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.