Mara nyingi sana utamsikia mtu anasema simu yake imekufa au imeharibika gafla jambo ambalo sio kweli, Simu zetu huwa hazifi gafla ila kuna dalili za awali zinazopelekea mpaka simu kufa au kuharibika na pengine unaweza ukawa unaziona na kuzichukulia kawaida kuwa haziwezi kuwa na madhara yoyote kwenye simu yako.
Simu yoyote ile kabla haijafa yaani kushindwa kufanya kazi kabisa lazima itaonesha dalili fulani fulani, lakini kwakua wengi hua tunazipenda simu zetu tunaishia kuona ni jambo la kawaida mpka pale itakapotokea simu imezima kabisa au inawaka ila haifiki mwisho (bluescreen of death ), kuna dalili za awali kuashiria simu yako kuharibika au kutofanya kazi (kufa).
1. Uwezo wa kutunza chaji kupungua sana(Reduced batty life).
Simu ikianza kupoteza uwezo wa kutunza chaji ni dalili mojawapo kuwa simu imeanza kupunguza ubora wake na uwezo wa matumizi, Kwa simu kama iPhone imekua rahisi kujua maendelo ya betri/battery yako kwa kuangalia “battery health“ kwenye Mipangilio/Settings ya simu hapo utaaona afya ya betri lako kwa asilimia, na unapoona simu yako inawahi kumaliza chaji au inatumia mda mrefu kujaa pasipo kawaida na inawahi kuisha basi hizo ni dalili za simu kuharibika.
Ushauri:
Tatizo hili unaweza kulitatua kwa kuweka betri mpya, unapoweka betri mpya jaribu kuwa makini na hakikisha unaweka betri nzuri ili kuepusha usumbufu.
2. Kupungua kwa uwezo wa ufanyaji kazi.
Simu inapungua uwezo wa ufanyaji kazi, kama ni kufungua programu flani itachukua mda mrefu au kufanya kazi nyepesi basi itachukua mda kuliko kawaida, sababu kubwa inaweza kuwa ni kukosekana kwa nafasi ya kutosha au vifaa vya simu (hardware) vimepitwa na muda yaani (outdated) au programu endeshi ni ya zamani sana.
3. Simu kuchemka isivyo kawaida.
Simu kuchemka sana ni sababu ya kuwa kuna vifaa havifanyi kazi ipasvyo, unakuta simu inachemka sana mpaka inaunguza au mda mwingine inakupa ujumbe/alert massage kuwa simu imechemka sana hivyo uiache ipoe. Hii inaashilia kuwa kuna kifaa kinashindwa kufanya kazi (hardware failure).
4. Simu kujizima mara kwa mara.
Simu kujizima mara kwa mara imekuwa ni sababu kuu ambayo hufanya simu kushindwa kufanya kazi kabisa, simu kujizima mara kwa mara husababishwa na mifumo (software) kuharibika au vifaa vya simu (hardware) kushidwa kufanya kazi ipasavyo.
5. Kuharibika kwa simu (physical damage).
Simu inaweza kupata hitilafu mfano kudondoka na kuvujika kioo au simu kuingiwa na maji au hitafu nyingine na unaweza kuona simu inafanya kazi kama kawaida lakini baada ya mda itaanza kupunguza ubora wake.
No Comment! Be the first one.