Biashara ziko nyingi na za aina mbalimbali na kila siku zinaanzishwa biashara mpya lakini kwa wakati huo huo teknolojia pia inazidi kukua kila siku, na teknolojia hii inaweza kukusaidia kukuza biashara yako na pengine kufikia malengo yako.
Kwa sasa watu wengi hununua bidhaa mtandaoni na imekuwa ni kawaida kufanya hivyo sababu ya kuepusha usumbufu wa kwenda dukani kuchagua bidhaa flani aipendayo, Kitu cha kwanza angalia unafanya biashara gani pia wateja wako wengi ni watu wa akina gani au umri gani, halafu fuata yafuatayo.
1. Uuzaji na matangazo (Marketing and advertising)
kwa sasa watu wengi wanatumia mitandao ya kijamii kupata taarifa na habari mbalimbali, mitandao ya kujamii kama Facebook, Instagram, Twitter, TikTok n.k pia mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya kufanyia biashara, biashara nyingi zinafanyika kwa kuweka tangazo la bidhaa yako kwenye mitandao ya kijaa endapo mteja amependa bidhaa yako basi atakutafuta ili aweze kununua. Mitandao ya kijamii ni sehemu muhimu sana kuitumia kufanyia biashara.
2. Tengeneza tovuti (website) ili kukuza biashara yako.
Tovuti (website) ni sehemu muhimu sana ya kutangaza bidhaa zako na kufanya biashara mtadaoni, tovuti ni sehemu ambapo utaeleza kwa kina aina ya biashara unaifanya na huduma unazotoa, tofauti na mitandao ya kijamii mabapo unaweka matangazo pekee na maelezo mafupi ya huduma au bidhaa yako, tovuti ni sehemu pekee mtu atapata maelezo ya kina kuhusu bidhaa, huduma zako na maelezo mengine muhimu ya biashara zako, ni rahisi kwa mteja kukuamini endapo bidhaa zako zimeelezewa kwa kina kwenye tovuti.
3. Kuza biashara yako kwa kutengeneza vipeperusi, kadi za biashara na mabango.
Vipeperushi (flyers), kadi za biashara (Business cards) au mabango (posters) ni moja ya njia bora ya kutangaza biashara yako kwa watu mbalimbali, lengo ni kuifanya biashara yako ikue na ijulikane zaidi na hii ni moja ya njia nzuri ya kutengeneza wateja.
4. Kuwa mbunifu kwa kuruhusu malipo kwa njia ya Mtandao (online transaction).
Kama umetengeneza tovuti (website) au programu (application) kuhusu biashara au huduma zako jitahidi uweke huduma ya malipo ka njia ya mtandao ili iwe rahisi kwa mtu kulipia huduma au bidhaa flani kuliko kumfanya mteja atumie njia zingine za malipo ambapo hufanya kupoteza wateja.
5. Tumia mifumo ya mapato na manunuzi.
Mfano una duka kubwa (supermarket) au biashara zingine ni bora ukawa na mfumo wa kuratibu bidhaa zinazoingia na kutoka, agizo (orders) za wateja, bidhaa zilizolipiwa, mapato na matumizi. Hii itakusaidia kendesha biashara yako vizuri sababu ya udhibiti mahiri wa taarifa zote za biashara yako.
6. Huduma kwa wateja (customer services).
Watu wengi huona “Huduma kwa wateja” kama ni sehemu ndogo sana ya biashara, lakini hii ni sehemu kubwa sana ya kukuza na kuleta wateja kwenye biashara yako, mteja anahitaji kusikilizwa, kuelemishwa na kupatiwa ushauri juu ya bidhaa flani, kama una toa huduma nzuri kwa wateja wako ndiyo utakavyozidi kupokea wateja wendi zaidi.
Unaweza kuweka sehemu ya maswali na majibu kwenye Tovuti (website), mitandao ya kijamii ili mteja anapouliza kupatiwa msaada hii itaongeza ufanisi zaidi katika biashara yako.
Teknolojia imekuja kurahisisha vitu vingi sana na hasa kwenye biashara zetu za kila siku, kadri unavyoitumia teknolojia vizuri ndiyo namna unazidi kukuza biashara yako/zako. ikiwa watu wengi kwa sasa hupenda kutembelea maduka ya mtandaoni na ni mhimu kwa mfanyabishara kuwa na duka la mtandaoni.
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.