Tanzania ukiilinganisha na Uganda/Kenya kuhusu uelwewa wa teknolojia inayowezesha miamala salama kuhusu suala zima la sarafu za kidijitali tupo nyuma lakini kwenye kongamano la pili (AIPC 2018) Blockchain Tanzania watatuelimisha siku hiyo.
Kama moja kati ya wale watu wanaosubiri kwa shauku kubwa kuweza kuhudhuria kongamano la kila mwaka kwa wadau na wana TEHAMA nchini Tanzania, namuomba mwenyezi Mungu anisaidie nisiweze kukosa hata siku moja ili niweze kusikia ambayo yapo, yanayoendelea kwenye teknolojia kwa upana wake.
Mtoa mada siku hiyo ni Jumuiya ambayo imeazimia kuwafanya Watanzania waweze kuelewa, kuamini na hata kuwekeza kwenye upande huo wa teknolojia ambao unaonekana kuvutia mataifa mengi duniani.