fbpx

Bei simu inayokunjika kutoka Samsung

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung inatuweka tayari na simu inayokunjika kutoka kwao ambapo tayari ulimwengu unafahamu machache kuhusu hicho ambacho kitaletwa kwenye ulinngo wa ushindani.

Samsung kama moja ya kampuni nguli inatazamiwa kurudisha teknolojia ambayo ilitoweka kwa miaka mingi lakini hivi sasa ikiwa na teknolojia kwa maana ya kwamba ni ulimwengu uliotawaliwa na simu janja.

Ambacho ulimwengu walikuwa hawajakijua ni simu hiyo itauzwa liasi gani? Kwa kweli kama una matarajio ya kuinunua itakapotoka basi inakubidi ujipange vilvyo kwani bei yake sio ndogo wala ya kubeza hata kidogo.

Imeelezwa kuwa simu hiyo itagharimu $1,700|Tsh. 3,310,000 na ikiaminika kuwa itaitwa “Galaxy F” ambayo itatoka pamoja na Galaxy X mwezi Machi mwaka 2019.

simu inayokunjika

Simu janja ya kwanza kutoka Samsung ambayo inakunjika.

Vipi bei ya simu inayokunjika imekushtusha? Sisi kazi yetu ni kukuhabarisha, kushauri halafu uamuzi utafanya wewe mwenyewe kwa utashi wako.

Vyanzo: Engadget, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Soko la simu janja Afrika: Transsion (Tecno, Infinix & Itel), Samsung na Huawei ndio wanaongoza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.