fbpx

Oreo yafika kwenye Samsung Galaxy J7 Prime

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sio simu zote za Samsung zimepata au zitapata masasisho ya programu endeshi toleo la nane maarufu kama Oreo lakini kwa  wanaotumia Samsung Galaxy J7 Prime watafurahi kwani sasa wanaweza kuhamia kwenye Android 8.

Katika mpango wa Samsung kupeleka masasisho ya programu endeshi ilibainisha simu ambazo zilitoka mwaka 2016 zilizo na progragramu endeshi-Marshmallow zitapokea masasisho na kuweza kuhamia toleo la Oreo.

Kabla hujafikiria kuhamia kuhamia kutoka toleo moja hadi jingine ni muhimu sana kuhakikisha simu/kifaa husika kina chaji angalau 50% na kuendelea, mpangilio wa intaneti uko sawa lakini kubwa zaidi kuwa na kifurushi cha intaneti zaidi ya 1024MB (1GB).

Masashisho ya Oreo kwenye Samsung Galaxy J7 Prime utegemee kuona maboresho kwenye muonekano wa vitu kwenye uso wa mbele, kipengele cha Smart View, Samsung Cloud, n.k. Kushusha/kuhamia kwenye Android 8 kitu chote kina ukubwa wa 1040MB (zaidi ya GB 1).

Samsung Galaxy J7 Prime

Taarifa ya kwamba unaweza ukapakua toleo la Android 8.

Sasa kama ulikuwa unasubiri simu yako (Samsung Galaxy J7 Prime) iweze kupokea masasisho hayo ni wakati wako kuhamia ila kwa kuzinngatia vitu muhimu ambavyo tumevielezea.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu janja: Zifahamu Oppo A9 na A9x
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.