ES Explorer ni moja ya app muhimu kuwa nazo kwenye android yako. ES Explorer inatumika kupekua na kushghulikia na mafaili ya aina nyingi kwenye kifaa chako au hifadhi nyingine kwenye mtandao.
Kwa maana hiyo, unaweza kutengeneza, kutazama, kurekebisha au kufuta mafaili kwenye simu, tableti au hata kompyuta iliyokuwa kwenye mtandao wa eneo la karibu (LAN) au kwenye mtandao wa intaneti na pia mafaili yalio kwenye hifadhi pepe kama Dropbox, Google Drive na Microsoft One Drive.
Mbali na kufanya hayo mambo ya msingi, Es Explorer inaweza pia kutumika kufanya yafuatayo:
- Kucheza muziki na video za kwenye simu
- Kucheza muziki na video kutoka kompyuta iliyo kwenye mtandao (kutumia kompyuta kama ‘media server’)
- Kufungua picha za aina mbalimbali kwenye simu au kutoka kwenye kompyuta.
- Kutuma ‘app’ kwenda kwenye simu/tableti nyingine au kompyuta.
- Kutuma picha, video, muziki, nyaraka na mafaili mbalimbali kutoka kwenye simu kwenda kwenye simu/tableti nyingine au kompyuta.
- Kutazama na kubadili ruhusa za mafaili kwenye simu zilizofunguliwa vikwazo (root explorer).
- Kuficha mafaili yasionekane na mtu mwingine.
- Kuweka recycle bin ya kukunusuru iwapo utafuta kitu unachohitaji kwa bahati mbaya.
- Kuchunguza mafaili yanayojaza nafasi kwenye simu au tableti na kuyashughulikia moja baada ya jingine au kwa mkupuo.
- Huduma ya FTP kwenye simu.
Es Explorer ina mambo mengi mengi zaidi kiasi cha kuifanya ipakuliwe zaidi ya mara millioni hamsini kwenye soko la Google Play Store. Programu hiyo imekuwepo kwa muda mrefu na toleo la sasa ni la tatu katika historia yake ila bado imefanikiwa kushika chati na kuaminika na watu wengi wa kawaida na wajanja wa Android.
Ushindani mkubwa kwa app hii ni Astro File Manager ambayo inajikita zaidi kwenye kurahisisha kushughulikia mafaili ya kwenye hifadhi pepe na kwenye kompyuta ya karibu kupitia simu. Ingawa Astro nayo inatamba kwa uwezo na muonekano wake, huduma ya ziada ya kicheza muziki na video ambacho ES explorer inakuja nayo kinaiweka ES explorer kuwa juu. Kicheza muziki hicho kina uwezo wa kucheza muziki moja moja au kwa mkupuo kutoka kwenye hifadhi ya mbali na hivyo kuweza kufanya kompyuta yako ya karibu kuwa ‘media server’.
No Comment! Be the first one.