fbpx

Apple, apps, Telegram

App Store: Apple waiondoa app ya Telegram kwenye soko lake la Apps

app-store-apple-waiondoa-app-ya-telegram

Sambaza

Apple waiondoa app ya Telegram kwenye soko lake la Apps maarufu kwa jina la App Store. Inasemekana uamuzi huo umefanyika ghafla baada ya timu yake kugundua kuna kitu hakipo sawa kwenye app hiyo.

Taarifa hiyo ilitolewa na Bwana Pavel Durov, muanzilishi wa app ya Telegram, ambayo ni app maarufu hasa kwa watu wanaojali usalama wa kimtandao. App ya Telegram ndio ilikuwa app ya kwanza kuwa na viwango vya ubora wa juu wa usalama wa mazungumzo kupitia teknolojia mbalimbali za usalama wa kidigitali zinazohakikisha mazungumzo ya watu yanakuwa salama dhidi ya udukuzi na kuchunguliwa na vyombo vya usalama.

Kwa kiasi kikubwa inaonekana app hiyo imetolewa baada ya kampuni ya Telegram kuanzisha pia toleo jingine la Telegram linalokwenda kwa jina la Telegram X ambalo ni bado lipo kwenye hatua ya mwanzo ya ubora.

Inaonekana kupitia app ya Telegram X kuna vitu ambavyo vimevunja utaratibu wa sheria za App Store. Moja ya sheria kali za Apple ni pamoja na kuhakikisha ya kwamba mtengenezaji app ahakikishe app ina mfumo wa kuchuja na kuzuia mazungumzo ambayo ni ya matusi au yanayoweza kudhuru – kama vile ugaidi.

SOMA PIA  Apple: Hivi Karibuni Utaweza Kuchaji iPhone na MacBooks Mara 1 Kwa Wiki

Telegram

Hadi leo bado Telegram huwa inajikuta katika kutoelewana na serikali nyingi duniani kw asababu ya jinsi teknolojia yake ya usalama ndani ya app yake inaweza kuwasaidia watu ata wasiokuwa na malengo mazuri kuweza kuwasiliana na kupanga mambo yao bila kuweza kunaswa na vyombo vya sheria.

App hiyo bado inapatikana kwenye Google PlayStore na wengi wanaamini inaweza kurudi kwenye soko la App Store ndani ya masaa kadhaa baada ya kampuni hiyo kufanya marekebisho yanayoitajika na Apple.

Je wewe ni mtumiaji wa app ya Telegram? Tupe mtazamo wako juu ya app hii.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Nickson