Google bado wanaendelea kujiimarisha sana katika swala zima la ulinzi na usalama hasa kwa wateja wao, sasa wamekuja na jipya katika Chrome.
Kingine pengine ambacho hukijui ni kwamba kila tarehe 28 mwezi wa kwanza makampuni yote ya kiteknolojia huwa yanasheherekea usiri, ulinzi na usalama wa taarifa za wateja wake na sasa Google wanazidi kuimerisha jambo hilo katika Chrome.
Mara kwa mara makampuni ya kiteknolojia yamekua yakihakikisha kuwa yanalinda taarifa za wateja wake kwa gharamu yeyote lakini vipi kwa kampuni ambazo zinamiliki vivinjari (browser)
Vitu kama unaswaji wa sauti, kamera na hata taarifa ya eneo ambalo upo ni vitu vya siri ukiwa unazunguka zunguka katika mtandao sio?
Kwa sasa kampuni ya Google kupitia kivinjari chake cha Google Chrome imekuja na kipengele katika huduma yake ya incognito –ile huduma ya kutumia chrome bila kuacha taarifa yoyote nyuma—ambacho kitasaidia zaidi taarifa hizo kubaki kuwa za siri zaidi.
Kipengele hicho si kingine bali ni uwezo wa kuzi’lock tab ambazo ziko katika hali ya incognito. Yaani hapa kinachotokea ni kwamba kama unatumia incognito katika kifaa cha android alafu ukatoka bila kufunga tab hiyo ..
…basi kaa ukijua ukirudi tena katika kivinjari ili kuingia tena katika Tab hiyo hiyo basi itakualzimu kwanza kuweka neno siri au hata kuweka passcode ambayo unatumia katika kifaa hicho ili kuendelea kutumia tab hiyo.
Ili kuwezesha hili ingia katika Chrome na kisha nenda katika Settings >> Privacy Security >> kisha washa ‘Lock incognito tabs when you close Chrome’
Mpaka hapo nadhani umeshajua namna ya kuwezesha hili, kumbuka njia hii itakuwezesha kuweza kuperuzi katika mtandao kwa siri bila ya kuacha taarifa zako nyuma hivyo kukufanya kuwa salama ziadi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii umeipokeaje? Je unahisi kipengele hiki kina mashiko sana? Au hakukua na haja ya kuwa na kipengele hiki kwa sasa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.