Hapa kuna mambo mengi sana lakini makubwa ni kwamba Amazon inafuga duka lake la vitabu hivyo vya kimtandao na ukiachana na hilo hata bado wataacha kabisa kusambaza vitabu hivyo.
Taarifa hii imetolewa na kampuni yenyewe (Amazon), kupitia katika akaunti ya ofisi ndani ya WeChat.
Hii ni kusema kuwa kuanzia mwezi juni 2023 watumaiji/wateja wote hawatakua na uwezo kununua vitabu hvyo na pia Amazon watatoa App ya Kindle katika masoko ya Apps huko China.
Amazon wanasema kuwa wamefanya hivyo lakini sababu sio kuhusiana na shinikizo la serikali au chochote kinachohusiana na siasa.

Biashara zingine zote – kama vile za matangazo, uhifadhi wa kimtandao (Cloud) na biashara yake ya kimtandao — za ndani ya nchi (China) zitaendelea kama kawaida.
Ukaichana na hayo bado Amazon inasema kuwa bado imejikita sana katika wateja wake wa huko nchini china.

Tamko lao ni kwamba wamerudi nyuma kidogo na kujitathimni ili kuhakikisha kuwa watakuja na huduma bora katika soko hilo la China.
Kumbuka Amazon pia ni moja kati ya makampuni makubwa sana ambayo kwa namna moja ua nyingine wamejitoa au wametoa sehemu ya biashara yake katika soko la China.

Kwa siku za hivi karibu makampuni kama Yahoo, LinkedIn na Airbnb zimejitoa au zimetoa sehemu ya bishara yao huko China.
Si mara ya kwanza kuona makampuni mengi yapunguza uhusiano wake kwa kupunguza au kuachana na baishara kabisa na China.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katiake eneo la comment, je udhani china ina shida gani kubwa maana sio mara ya kwanza makampuni mengi kuachana na nchi hiyo.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.