fbpx

Aliyepooza anaweza akatembea tena

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sijui lini nitaacha kusema kuwa teknolojia huwa inaangazia aliye mlemavu na asiyekuwa mlemavu kwa kuamini kuwa hata yule mwenye ulemavu anaweza akatumia kama makundi mengine ya watu. Mifano ipo mingi na mmojawapo ukiwa aliyepooza kuweza kutembea tena.

Mtu aliyetooza ni nani?

Ni mlemavu ambae ukimgusa sehemu fulani ya mwili wake hawezi kuhisi kuwa kitu kipo juu ya ngozi yake na tatizo hili linasababishwa na hitilafu kwenye uti wa mgongo pia kupooza kwa mtu/mnyama inaweza kuwa ni mwili mzima au sehemu/kiungo fulani ndio kimepooza.

Daima nimekuwa nikivutiwa sana pale nianapoona teknolojia inasaidia kurudisha furaha kwa mtu ambae ana matatizo hasa mlemavu kwa jinsi mambo yanavyozidi kupanuka wataalaam hawachoki kufanya tafiti na kufanya majaribio ya kitu fulani.

Kimetengezwa kifaa ambacho kinawekwa kwenye sehemu ambayo imeathirika sana ndani ya uti wa mgongo na hatimae kupeleka taarifa kwenye ubongo ambapo itarudisha majibu na kuamuru mtu kunyanyua mguu/kupiga hatua.

Aliyepooza

Matumaini ya mgonjwa wa aliyepooza kuweza kutembea huenda isiwe ndoto tena.

Ukweli uliopo nyuma ya kumfanya mgonjwa aliyepooza kutembea.

Kitu ambacho kifaa hicho kinafanya ni kushtua mishipa ya fahamu kisha kupeleka taarifa kwenye ubongo na hatimae majibu kurudi na yatasabisha mgonjwa kuweza kufanya kitu fulani kulingana na taarifa iliyotolewa.

Aliyepooza

Kifaa hicho kimeonyesha matokeo chanya na si tu kwa panya bali hata kwa binadamu aliyepooza.

Mpaka sasa wagonjwa watatu waliojitolea wameshawekewa kifaa hicho na majaribio ya awali yanatoa matumaini ingawa mazoezi yanahitajika ili kushtua/kujenga misuli ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haitumiki.

Vyanzo: Extreme Tech, Aljazeera

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.