fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Tanzania

Akaunti ya Facebook ya Meya Jerry Silaa Yawa ‘hacked’!

Akaunti ya Facebook ya Meya Jerry Silaa Yawa ‘hacked’!

Spread the love

Jerry SlaaAkaunti ya Facebook ya Meya wa Ilala ‘imehackiwa’! Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram Meya Jerry Silaa adai kuna mtu aliyetumia akaunti hiyo na kutuma ujumbe kwa marafiki zake ‘akidai’ anamaongezi nao ya siri.

Ujumbe alioutoa Instagram

Watu wengine walikuwa wanauliza, ‘hata wewe wanakuhack’… Kwa kifupi ni muhimu sana kuwa mwangalifu na anuani (linki) zozote unazotumiwa kupitia sehemu yako ya ujumbe wa siri Facebook. Uliza anuani hiyo inahusu nini, hii itasaidia kwani kama mtu hakukutumia itakuwa ni rahisi yeye kukujibu na hivyo kugundua kuwa akaunti yake imeathiriwa, kwa kila mwingine anavyobofya ndivyo ujumbe huo unavyoenea kwa wengine na wengine. Kujua zaidi kuhusu suala hili soma makala ‘ JIEPUSHE Na Ku’click ‘Link’ Zisizo Na Maana Kwenye Mitandao Ya Kijamii’ – bofya hapa!

SOMA PIA  Facebook M: Msaidizi Anayefanya Kazi Kama Ile ya 'Siri' au 'Google Now'

Timu nzima ya Teknokona inampa pole Mheshimiwa Meya, cha kushukuru hakuna cha ajabu kilipostiwa kwenye akaunti yake.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania