fbpx

Simu za Google Pixel zapata muonekano wa giza

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

Sambaza

Google wanajivunia sana kutokana na simu za Google Pixel ambazo zilipata mapokezi mazuri na kuifanya Google kujipatia kipato kizuri lakini pia kuiweka kwenye ramani ya ushindani kuhusu simu janja.

Kwa mwaka na zaidi sasa habari za makampuni kuweka kipengele cha “Muonekano wa giza” kwenye programu tumishi, tovuti n.k sio jambo geni sana kwa wengi, Google ambao ndio wenye simu zinazoitwa Google Pixel (Pixel 2, 2XL, 3, 3XL) wameamua kuleta masasisho ya ulinzi kwa mwezi Machi ambayo yanajumuisha muonekano wa uso mbele kwenye simu kuwa giza pamoja na kuweza kuona ni asilimia ngapi ambazo zimeshashushwa.

Kwanini muonekano wa giza?

Hilo ni swali ambalo naamini kwa yeyote ambae anapenda kujua vitu vya kidijiti atakuwa ameshajiuliza mara kadhaa na pengine akakosa jibu lakini fahamu kuwa utakapokuwa umeamua kutumia muonekano wa giza basi unaifanya simu husika kutunza chaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kwamba mwanga utakaokuwa ukitumika ni mdogo sana/usitumike kabisa.

Simu za Google Pixel

Masasisho ya mwezi Machi kwa simu za Google Pixel ambayo yanajumusha kuwa muonekano wa giza.

Unaweza ukawa unapenda kuweka simu yako kwenye muonekano wa giza lakini ikawa changamoto kutumia prgramu tumishi fulani fulani ambazo nazo zina mbwembwe kama hizo. Sasa maamuzi ni yako lakini kiujumla kwenye Android 9 kipengele hicho kipo.

Chanzo: Android Police

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Huawei yashikwa kwa picha Feki, ujio wa simu yake mpya ya P30 PRO
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.