Kurasa ndani ya Facebook zimekuwa lukuki na pengine na pengine kugeuka kuwa kera kwa yule anayeziangalia hivyo kufanya maamuzi ya kufuta ukurasa Facebook lakini ikwa shida kidogo kwake.
Ugumu utatokea pale tu iwapo mtu anayetaka kufuta ukurasa husika si kiongozi (admin) kwa lugha nyingine mtu huyo ana cheo tofauti na kile ambacho kinampa nguvu ya kuweza kufuta kurasa yoyote ndani ya Facebook iwapo tu yeye ndio mwenye wadhifa wa juu kabisa.
Kwa yule ambae ana madaraka ya kuweza kufuta ukurasa basi anaende kwenye mpangilio (settings) kisha aangalie kipengele cha mwisho kabisa kutoka kwenye ukurasa mpya utakaofungunguka (remove page).
