Mtandao wa kijamii unaojihusisha sana na mambo ya video kwa ujumla umekiri kwamba kuna tatizo la kiufundi katika App yake ya iOS lakini ni kwamba hili jambo wanalishughulikia.
Tatizo hili halijamkuta kila mtu ambae anatumia mtandao wa Youtube katika kifaa cha iOS, ni baadhi ya watu tuu ambao wamefikwa na jambo hili.
Youtube ndio mtandao wa kijamii maarufu zaidi kuliko mingine ambao unajihusisha na kusambaza maudhui kwa njia ya video. Ukiachana na umaarufu huo ni bado kampuni inajitahidi kuhakikisha kuwa inawaletea wateja wake kile kilicho bora na pia kutatua baadhi ya changamoto katika App hiyo.
Sio mara ya kwanza kwa mitandao mikubwa ya kijamii kukutwa na mambo kama haya hata mtandao wa WhatsApp ulikutwa na adha kama hii wiki iliyopita.
Kilichokua kinafanyika katika App hii ni kwamba maelfu walilalamika kuwa App hiyo ukiifungua tuu haifanyi kazi na kisha kijifunga.
Wengine walisema kuwa walipata na ujumbe kabisa wakati wamefungua App hiyo ambao unasema “A serious error occurred” kwa tafsiri ya haraka haraka ukiwa na maana kuwa kuna hitilafu ya msingi imejitokeza.
Kizuri ni kwamba Youtube wenyewe walikiri jambo hili na wameweka wazi hilo jambo katika baadhi ya mitandao ya kijamii
hi, we're aware that many of you using the YouTube app on iOS devices may be experiencing crashes
we're so sorry about this & have begun working on a fix! updates soon🔍
— TeamYouTube (@TeamYouTube) November 30, 2022
kizuri ni kwamba matatizo kama haya yakitokea katika mitandao ya kijamii wamiliki huwa wanafanya juu chini ndani ya muda mfupi hali irejee kuwa salama ili watu waweze kufurahia mtandao huo kama kawaida.
Tuna imani kuwa tatizo hili halitachukua muda mwingi na kutatuliwa na mamlaka husika kutoka katika mtandao wa kijamii wa Youtube
ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je wewe ni mtumiaji wa iOS au umesikia lolote kwa ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na jambo hili?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.