Windows 7 hivi sasa ndiyo programu ya mfumo wa uendeshaji (operating System) maarufu zaidi duniani kwa namba ya watumiaji, kulngana na ripoi iliyotolewa hivi karibuni jamshirika la Application Net.
Katika mwezi Agosti, Windows 7 inamiliki 42.76% ya soko, ikiiacha Windows XP kwa udogo sana kwani Windows XP inamiliki asilimia 42.52. Windows Vista imeketi nafasi ya tatu kwa kushikiria asilimia 6.15 ya soko, ikifuatiwa na Mac OS X 10.7 na Mac OS X 10.6 kwa 2.45% na 2.38%, kwa mtiririko huo.
Yote katika yote, hii inamaanisha bidhaa za Microsoft inadhibiti baadhi ya asilimia 92 ya soko.
Imechukua miaka mitatu kwa ajili ya Windows 7 kushika nafasi hii. Windows 7, ambayo ilizinduliwa Oktoba 2009, hivi karibuni itafuatiwa na toleo jipya kutoka kampuni ya Microsoft – Windows 8.
Windows 8, ambayo imepangwa kuingia sokoni hapo Oktoba 26, itakuwa programu ya mfumo wa uendeshaji ya kwanza kutoka Microsoft iliyotengenezwa kufanya kazi vizuri kote kwenye vifaa vya tableti na kompyuta za mezani pamoja na laptop.
Watumiaji wa Windows XP, Vista au Windows 7 wataweza kuboresha (upgrade) kwenda Windows 8 Professional kwa dola 39.99 za kimarekani, (takribani Tsh 65000) kupitia kushusha (download) mtandaoni.
Windows XP Imekuwa Maarufu Zaidi Pale Windows Vista Haikupokelewa Vizuri! |
Windows 8 Itatoka Mwezi Ujao |
No Comment! Be the first one.