fbpx
Kompyuta, Windows 10

Windows 10 imefikisha watumiaji milioni 700

windows-10-imefikisha-watumiaji-milioni-700
Sambaza

Kampuni ya Microsoft imetangaza kuwa kwa sasa kuna karibu kompyuta milioni 700 zilizounganishwa na Windows 10.

Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft, Satya Nadela alisema hayo katika mkutano wa wanahisa wa kila mwaka kwamba kuna zaidi ya kompyuta milioni 600 zilizounganishwa na Windows 10. Microsoft Windows ndio mfumo endeshi maarufu zaidi duniani wa kompyuta na hakuna dalili yoyote ya kupungua kwa matumizi yake kwa muda wa karibuni.

INAYOHUSIANA  Pokea na jibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia kompyuta

Mwaka 2017, Microsoft ilitangaza kuwa kuna kompyuta milioni 600 zinazounganishwa kila mwezi kuwa na mfumo wa Windows. Mifumo ya Windows ambayo bado inatumika kwa watu wengi ni Window XP, 7, 8 na 10.

watumiaji milioni 700
Muonekano Wa Windows 10

Idadi ya kompyuta zinaotumia Windows 10 ni ya kushangaza kwa programu endeshi kufikia idadi hiyo huku ikiwa na miaka mitatu tu tangu kuzinduliwa kwake. Mwaka 2018, Microsoft imetabiri kompyuta bilioni moja zitatumia Windows 10.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.