fbpx

Pokea na jibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia kompyuta

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tunatumia simu zetu kufanya mawasiliano kwa njia tofauti tofauti na kuweza kupata majibu (mrejesho) muda huohuo au baada ya dakika kadhaa kupita.

Teknolojia inakuwa ma sasa unaweza kupokea, kujibu ujumbe ulitumwa kwenye simu yako kwa kutumia kompyuta. Google waleta kitu kipya ambacho utaweza kuunganisha simu yako na kompyuta, hivyo kuweza kujibu ujumbe mfupi wa maneno ulitumwa kwenye namba yako ya simu.

Kitu hiki (Messages for Web) ni kwa wale wote wenye kutumia simu janja zinazotumia mfumo endeshi wa Android na vitu ambayo ni lazima uwe navyo/kuvikumbuka ni namba yako ya simu na simu rununu iwe na uwezo wa kudaki (scan) lakini pia kompyuta inayoshika mtandao (intaneti).

ujumbe mfupi wa maneno

Hatua kwa hatua jinsi ya kuunganisha simu kwenye kompyuta ili uwe na uwezo wa kupokea na kujibu kupiyia kompyuta.

Messages for Web inaweza kuonekana kufanana na jinsi ambavyo mtu anatumia WhatsApp kwenye kompyuta lakini ni muhimu sana kujua tofauti ya WhatsApp Web na Messages for Web.

Tofauti kati ya Messages for Web na WhatsApp Web.

  • Moja, si lazima simu iwe hewani upande wa intaneti ili upande wa pili (kompyuta) uweze kupata na kuweza kujibu ujumbe  uliotumwa lakini ni lazima simu iwe hewani,
  • Pili, namba yako ya simu uwe unaifahamu kwani bila ya hiyo vifaa hivyo viwili havitaweza kuwasiliana.

Anza sasa kujibu ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwa mfumo ulizoeleka kwa kutumia kompyuta>>>BOFYA HAPA.

Messages for Web inaweza kuwa msaada sana kwa yule ambae muda mwingi anakuwa karibu na kompyuta kuliko na simu hivyo kuweza kufanya mawasiliano kwa njia ambayo itamfanya mtu asichukue muda mwingi sana kuangalia kilichojiri kwenye simu.

Vyanzo: ARS Technica, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Sony Xperia 1: Simu yenye upekee wa aina yake
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.