WhatsApp inazidi kukua kwa kasi na Facebook wanaringa kwelikweli kwani wanajitahidi kuwaonesha wawekazaji ya kwamba uamuzi wa kununua kampuni hiyo ya WhatsApp ulikuwa muhimu na wenye faida.
Katika kuonesha hili Facebook wamekuwa na utamaduni wa kuonesha data mbalimbali zikionesha ukuaji wa mtandao huo na mwezi huu wameonesha data zao za ukuaji.
Data hizo zinaonesha watumiaji wa WhatsApp kwa mwezi umepanda kutoka wastani wa takribani watumiaji milioni 600 hadi kwenda watumiaji milioni 700 kwa sasa.
Hii inaonesha ukuaji wa takribani watumiaji milioni 200 tokea Facebook waliponunua kampuni hii.
Kwa sasa kuna wastani wa meseji bilioni 30 zinatumwa kila siku kutumia WhatsApp.
Ukuaji wake katika wastani wa watumiaji wa huduma kwa mwenzi umeifanya WhatsApp kuwa kileleni kuzidi huduma zingine za kijamii kama vile Twitter (Watumiaji milioni 284 kwa mwezi) na Instagram ikiwa na watumiaji milioni 300 kwa mwezi wa Disemba 2014. Kwa sasa WhatsApp imepitwa na Facebook, kampuni mama, ikiwa na wastani wa watumiaji bilioni 1.3 kila mwezi.
Fahamu mambo na ujanja mbalimbali katika kutumia WhatsApp -> HAPA!
No Comment! Be the first one.