Pengine hii ni moja kati ya sasisho ambalo ni muhimu sana katika kipengele cha makundi katika mtandao wa WhatsApp, lakini je kwa namba hii je kutakua na maelewano kweli?
Ni mara nyingine tena mtandao wa kijamii wa WhatsApp unajikita katika kuhakikisha kuwa unakuja na vipengele kadha wa kadha ambavyo vitasaidia kampuni hiyo kufurahisha mioyo ya watumiaji wake.
Habari hii imekuja baada ya kampuni kutangaza huduma ya WhatsApp premium kwa baadhi ya watu ambao wanatumia huduma ya WhatsApp business.
Kwa sasaa kipengele hicho kipo katika majaribio kwa baadhi ya watumiaji (waliochaguliwa) wanaotumia Android na iOS.
Licha ya kuwa watu 1024 ni wengi sana lakini pata picha kwa mfanya biashara hii itakua ni jukwaa kubwa kabisa kwa wateja wake kuweza kuona bidhaa na vile vile kutoa mrejesho wao n.k
Ni wazi kuwa namba hiyo ni kubwa sana lakini kama kundi likiwa na sheria thabiti ambazo zinaliongoza kundi hilo basi kila kitu kitaenda sawa.
Ni wazi kuwa mtandao huu wa WhatsApp ni bado unaboresha sana huduma zake na kuendelea kutoa vipengele vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vitawazidi watumiaji wake wazidi kutumia mtandao huo na pengine kuzidi kupata watumiaji wapya
Chanzo: WABetaInfo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeiopokeaje? Je uko tayari kuwa ndani ya kundi lenye watu 1024?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.