fbpx

Vidokezo vya kwenye Samsung Galaxy Note 9

1

Sambaza

Kwa wiki/miezi kadhaa sasa watu wengi wamekuwa wakijaribu kujua simu janja ya Samsung Galaxy Note 9 itakuwa na sifa zipi, hivi karibuni sifa nyingine zimejulikana!.

Samsung Galaxy Note 9 inatarajiwa kuzinduliwa mwezi huu wa Agosti na wiki chache zilizopita bei ya simu hiyo ilikwishafahamika hata kabla ya uzinduzi wa simu yenyewe ambayo inaaminika kuwa na maboresho lukuki:

Muonekano/Kioo. Kamera za watu ziliweza kuona Afisa Mkuu Mtendaji wa Samsung akitumia simu mpya na kwa haraka haraka inaaminika kuwa ni Samsung Galaxy Note 9 ambayo ni fupi na nyembamba zaidi kuliko watangulizi wake. Kioo chake kinaaminika kuwa na urefu wa inchi 6.4.

Alama ya kidole. Kwenye simu ya Samsung Galaxy Note 9 teknolojia ya kutumia alama ya kidole imehamishwa na kuwekwa chini kidogo ya kamera tofauti na hapo awali (kwenye Note 8) kipengele hicho kiliwekwa pembeni tu ya lenzi kitu ambacho kililalamikiwa na walionunua Samsung Galaxy Note 8 kwa kugusa lenzi badala ya kitufe cha alama ya kidole.

Samsung Galaxy Note 9

Hapo ndipo S-Pen itakapokuwa inawekwa.

Betri/Diski uhifadhi. Kwenye simu hii inaonekana kuwa na ongezeko la 700mAh na kufikia 4000mAh kwenye Samsung Galaxy Note 9. Memori yake ya ndani inaelezwa inaweza kuwa GB 512 na kuweza kukubali memori ya ziada ya mpaka TB 1.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy yenye 5G haipo mbali

S-Pen/Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni. Ile kalamu ya kidijiti ni moja ya sehenu ambayo inaaminika kufanyiwa mabadiliko ya aina yake na kuifanya simu hiyo kuvutia. Ulikuwepo uvumi kuwa Samsung ina mpango wa kuachana kuweka sehemu ya kuchomeka spika lakini kwa mujibu wa taarifa zilizovuja Samsung Galaxy Note 9 itakuw na sehemu hiyo ya kuchomeka spika.

Samsung Galaxy Note 9

Muonekano wa Samsung Galaxy Note 9 ukidhihirisha kuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni.

Kati ya vitu vyote imekuwa ngumu kufahamika kuwa kamera zake zitakuwa na uwezo gani ila TeknoKona hatutakuwa mbali na tutahakikisha tunawaletea uchambuzi wa kina na uhakika itakapokwa imezinduliwa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|