fbpx

Huawei ya pili kimauzo kwa mara ya kwanza

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Simu ya Huawei ya nchini Uchina imekuwa ya pili kwa mauzo ya simu duniani yaliyofanyika katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu na kuipiku kampuni ya simu ya Marekani, Apple.

Kwa muda mrefu Kampuni ya Huawei imekuwa nafasi ya tatu ya uuzaji wa simu nyingi duniani nyuma ya vinara Samsung na Apple kwa muda wa miaka saba.

Katika robo ya tatu kwa mwaka 2018 Samsung imeweza kuuza simu 71.9m sawa na 20% ya soko, Huawei wakiweza kuuza simu janja 54.2m ikiwa ni sawa na 15% ya soko lote na Apple wakiwa wameuza simu takribani 41.3m ambapo ni sawa na 12% ya soko lote.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Huawei imeweza kutawala soko la simu kwa robo ya pili ni baada ya kutoa simu mpya ya Huawei P20 Pro yenye vidokezo pekee ambavyo hakuna kwa simu zilizoko sokoni. Simu hiyo ya Huawei P20 Pro inayoelezwa kusaidia ukuaji huo iliingizwa sokoni Machi 2018.

Huawei ya pili

Huawei P20 Pro ina jumla ya kamera tatu zenye ukubwa wa 40MP, 20MP na 8MP huku Kamera yake ya mbele ikiwa na ukubwa wa 24MP. Simu hiyo inauzwa $1,050 sawa na Tsh. 2.3.

Ingawa Samsung imeongoza katika robo ya pili kwa mwaka 2018 lakini ndio kampuni iliyoshuka kimauzo kwa 10% ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka uliopita. Apple imeongeza mauzo yake kwa 1% na Huawei ikiwa kinara kwa kuongeza 41%.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Wadukuzi wanaweza wakafanya simu ikaishiwa na chaji
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.