fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao wa Kijamii Twitter

Twitter Imeachana Na Kutoa Tiki Ya Bluu Kwa Muda!

Twitter Imeachana Na Kutoa Tiki Ya Bluu Kwa Muda!

Spread the love

Unakumbuka hapo nyuma tuliandika kwamba kwenye mtandao wa kijamii maarufu wa twitter, mtu yeyote anaweza kuomba kupata tiki ya bluu.

Tiki hiyo angeweza kuipata kwa kujaza fomu maalumu, na kisha akafanyiwa uhakiki na mtandao huu na baada ya hapo anaweza kuipata au asiipate kulingana na jinsi twitter wenyewe walivyoona.

SOMA PIA  Twitter yafanya maboresho katika namna ya ku-tweet

Vile vile niliandikaga kuhusu twitter kutoa tiki  ya bluu kimakosa na hii unaweza kuisoma zaidi —> Hapa <—

Sasa baada ya hili sakata mtandao huo umeamua kusitisha kwa muda zoezi hili la kutoa tiki ya bluu kwa muda.

SOMA PIA  Nafasi za Kazi kuanzwa kutangazwa kupitia Facebook

Sababu ya msingi ambayo mtandao huu unaitoa ni kwamba inasema imefanya hivyo makusudi ili kuhakikisha kwamba inakiboresha kipengele hiki.

Tuwape muda tuone itakuaje….

Naomba niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania