Kwa muda mrefu watu wametaka uwezo wa kutuma na kupokea meseji kwenye Instagram web, yaani moja kwa moja kwenye tovuti ya Instagram.

Instagram wamezesha uwezo huo kwa sasa na unapatikana kwa watumiaji wake wote duniani kote. Kwa muda mrefu uwezo huo uliletwa na kubakia kwenye app tuu. Uwezo huu umekuwa unafanyiwa majaribio tokea mwezi wa kwanza mwaka huu.
Uwezo huu unaonekana unawalenga zaidi watu ambao wanasimamia akaunti za makampuni, waandishi wa habari na watu ambao wanajibu meseji nyingi kwa siku – kwani kujibu kwa kutumia keyboard za kompyuta ni rahisi na haraka zaidi ukilinganisha na kwenye simu.
Pia watu wataweza kutuma video, picha na emoji kama kawaida kupitia eneo hilo la kuchati.
Uwezo wa kupost moja kwa moja kupitia tovuti hiyo bado na inaonekana lengo halipo kabisa, ili kuhakikisha bado app inabadikia kuwa sehemu muhimu ya utumiaji.
Je wewe ni mtu ambaye unanufaika na uamuzi huu? Tuambie kwenye comment, endelea kutembelea Teknokona.