fbpx
Roboti, Teknolojia

Kipindi hichi cha Covid-19, Roboti wa kuchukua ajira za watu wapata umaarufu zaidi

covid-19-roboti-wa-kuchukua-ajira-za-watu-wapata-umaarufu
Sambaza

Kwa muda mrefu roboti wenye uwezo wa kuchukua ajira za watu wamekuwa wakipata pingamizi kutoka kwa makundi ya wafanyakazi na watu wanaoamini teknolojia ya roboti wa aina hii wataharibu soko la ajira kwa binadamu.

Makampuni yanayotengeza roboti wanaoweza kuchukua ajira za watu yanapitia katika kipindi kizuri zaidi katika kujitanganza. Inasemekana makampuni hayo yameongeza juhudi za kutafuta wateja na wakezaji katika kipindi hichi kwani bidhaa zao ndio zinaonekana kuwa suluhisho la muda mrefu iwapo tatizo kama la Covid-19/Corona likitokea tena.

Roboti wa kuchukua ajira za watu
Roboti wa kuchukua ajira za watu, hasa hasa katika eneo la ubebaji mizigo n.k.

Janga la Covid-19 limechangia na litaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa uhitaji wa utumiaji wa maroboti katika viwanda mbalimbali duniani.

Sababu kuu;

  • Roboti wataweza kufanya kazi ata pale ambapo wafanyakazi wengi watahitajika kutokuwepo kiwandani.
INAYOHUSIANA  Second Skin: Wanasayansi waja na Ngozi ya Bandia, Kuficha Uzee na Makovu!

Viwanda ambavyo kazi zake nyingi tayari zilikuwa zinafanywa na roboti havijaathirika sana kama vile viwanda ambavyo kazi nyingi zilikuwa zinahitaji wafanyakazi kuwepo.

  • Utegemeaji wa vipuli kutoka mataifa mengine umeonekana kuwa tatizo.

Tatizo la Covid-19 limefanya viwanda vikubwa vilivyokuwa vinategemea vipuli kutoka kwenye viwanda vya mataifa mengine kukosa vipuli hivyo kwa wakati na hivyo kuathiri utendaji wa viwanda vyao. Suala la Corona limeathiri kwa kikubwa pia sekta ya usafirishaji kati ya mataifa mbalimbali.

Kutokana na hili tayari makampuni ya utengenezaji wa maroboti wa viwandani wametembelea sana viwanda kama hivi kujaribu kuuza bidhaa zao ambazo zitahakikisha vipuli vinawezwa kutengenezwa kwa gharama nafuu kwenye viwanda husika bila kuwa na utegemeza kutoka viwanda vya mataifa mengine.

INAYOHUSIANA  Tanzania: Inashika nafasi ya 149 kwa kasi ya intaneti

Makampuni ya utengenezaji roboti yameanza kupokea uwekezaji mkubwa katika kipindi hichi.

Inaonekana wawekezaji wengi wameona makampuni ya utengenezaji wa teknolojia za roboti wa viwandani na wa kazi zingine, yatakuwa ni makampuni yenye faida kubwa hivi karibuni. Tayari wawekazi wameanza kuwezekeza pesa nyingi kwenye makampuni hayo.

Mifano:

  • ForwardX Robotics, Beijing.

Kampuni ya utengenezaji wa roboti kwa ajili ya sekta ya usafirishaji imepata uwekezaji wa dola milioni 15 katika kipindi hichi, na hivyo kukuza mtaji hadi kufikia dola milioni 40 (takribani Tsh Bilioni 92).

  • BrainCorp

Kampuni inayotengeneza roboti wa aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja roboti kwa ajili ya sekta ya afya. Kampuni hii imepata uwekezaji wa dola milioni 36 hivi karibuni (takribani Tsh Bilioni 83).

INAYOHUSIANA  Njia Tano za Kulinda Data Zako Sasa

Ata kabla ya Covid-19 tayari sekta hii ilitegemewa kukua kwa kasi hivi karibuni. Ujio wa janga utafanya ukuaji kuwa wa haraka zaidi na kufanya makampuni ambayo hayakuwa na lengo la kutafuta roboti kwa ajili ya baadhi ya kazi kufanya hivyo – na hii ita maanisha binadamu kupototeza ajira hizo.

Je una mtazamo gani kuhusu utumiaji wa roboti katika viwanda na maeneo mbalimbali kwa kazi ambazo watu wa kawaida walitakiwa kuajiriwa kabla? Soma zaidi kuhusu teknolojia na bidhaa za roboti -> Teknokona/Roboti.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |