Ngoja kwanza, sio hashtags kabisa lakini vile vile huwezi sema sio hashtag maana vipengele hivi vinafanana kabisa jinsi ya utumikaji.
Mtandao wa Threads umeweka wazi kabisa kwamba unakuja na kipengele hicho ambacho kazi yake dhahiri ni kuonyesha au kuweka wazi mada kuu kwa wakati huo kwa mfumo kama wa hashtags.
Kipengele hiki kitakua kinafanya kazi ambapo kitamfanya mtumiaji kuunganisha Thread yake na mada Fulani – ambayo inaweza kuwa imetumika na watu wengi sana.
Ukiwa unaanda Thread mpya utaweza kuingia katika alama ya # na kisha kuchagua mada moja wapo ambayo unaweza ukapost kitu kuhusiana nayo.
Na hapo utakua umefanikia kui’tag hiyo mada katika Thread yako – ni kama hashtag inavyofanya kazi sio?
Mtu akiingia katika mada iliyochaguliwa katika Thread atakutana na watu wengine wengi ambao na wao wamezungumzia mada hiyo – bado kama hashtag sio?
Kwa kifupi hii ni kama hashtag kabisa lakini yenyewe imekuja katika mfumo ambao huwezi kuweka alama ya # na kisha mada yako.
Threads ni mtandao wa kijamii ambao unamilikiwa na kampuni ya Meta na kwa sasa mtandao huo umekua ukifanyiwa maboresho kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa unawapa watumiaji wake kile kilicho bora.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni hii inaweza leta mapinduzi kwa hashtag tuliyoizoea?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.