Samsung ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika swala zima la kutengeneza na kuuza simu janja.
Samsung pia ndio kinara wa simu za kujikunja (fold na flip) ambapo kampuni ndio inashika usukani katika mauzo ya simu za aina hizo.
Teknolojia ambayo inatumika kutengeneza simu hizi ni ya hali ya juu na vile vile ina gharama zaidi katika kutengeneza simu ya aina hii.
Hali hii inapelekea katika simu za aina hii kutoka kwao iwe na bei kubwa kidogo kilinganisha na simu zingine kutoka katika kampuni hiyo.
Mara kwa mara kumekua na fununu za hapa na pale kwamba Samsung wana mpango wa kutengeneza simu za aina hii za bei nafuu.
Kumbuka kwa sasa simu kama Samsung Galaxy Z Fold 5 inafikia zaidi ya dola 1,800 za kimarekani hii inaonyesha kabisa ni jinsi gani zilivyo na bei kubwa.
Mzungumzaji wa kampuni hiyo ameweka wazi kabisa kwamba kwa sasa kampuni hiyo haina mpango wa kutengeneza simu za kujikunja za bei ya chini.
Kitu pekee ambacho kampuni itajitahidi katika simu za aina hii ni kuhakikisha kwamba wanalete simu za aina hii zikiwa na sifa za undani za aina yake hii ikiwa ni kuhakikisha kuwa mteja anapata thamani ya pesa zake.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa Samsung kutotoa simu za aina hii za bei ya chini kidogo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.