Unapata matatizo ya mshituko wa moyo alafu hakuna huduma ya haraka ya usafiri wa ‘Ambulance’? Kama upo Bongo basi ni majanga ila kama upo nchini Sweden basi ondoa shaka.
Uwezekano wa mtu kuishi baada ya mshituko wa moyo hupungua kwa asilimia 10 kwa kila dakika inayopita bila kupata huduma ya kwanza na matibabu yanayofuata. Kwenye nchi zilizoendela, wapo watu wengi wenye elimu ya huduma ya kwanza na mafunzo ya ‘CPR’ na wanaweza kusaidia lakini hawana taarifa ya mtu anayehitaji msaada.
Nchi ya Sweden imeweza kutatua kitendawili hiki cha uchelewashaji wa huduma ya kwanza kwa ‘ambulance’ kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari kama Stockholm na yenye watu wengi wenye ujuzi wa CPR lakini hawana taarifa ya wagonjwa kwa kutengeneza mtandao unaotumia mfumo wa jumbe mfupi (SMS) kwa kuwapa taarifa punde mgonjwa anapopata tatizo.
Mtu yeyote akipiga 112, ujumbe mfupi wa SMS unatumwa kwenda kwa watu wote waliojisajili kujitolea walio ndani ya mita 500 kutoka kwenye eneo la simu iliyopigwa. Mfumo huo umekuwa na mafaniko kiasi kwamba katika asilimia 54 ya matukio, watu wa kujitolea wamefanikiwa kufika na kutoa msaada kabla ya ambulance kufika. Kwa kutumia mfumo huu na njia nyingine za msaada, uwezekano wa kuishi baada ya mshituko wa moyo kwenye mji wa Stockholm umeongezeka kutoka asilia 3 hadi 11 ndani ya miaka kumi iliyopita.
Je, una nini la kusema kuhusu huduma kama hii kwako? Tuungane kwenye mazungumzo hapo chini.
Chanzo: howtogeek.com
No Comment! Be the first one.