fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Android 11 yafika kwenye Samsung Galaxy Tab A 8.0 (2019)

Android 11 yafika kwenye Samsung Galaxy Tab A 8.0 (2019)

Spread the love

Watumiaji wa Samsung Tab ni wengi duniani kote na tunapozungumzia programu endeshi kwa sasa basi ni lazima itakuwa Android 11. Taarifa iliyopo toleo hilo la Android limeshagonga hodi kwenye Samsung Galaxy Tab 8.0 (2019).

Samsung imekuwa mstari wa mbele katika kutoa masasisho kwa simu janja zake zamu hii ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu Samsung Galaxy Tab 8.0 (2019) kuzinduliwa ikiwa na Android 9.

SOMA PIA  Kukosea namba ya mtu anayempigia kwamuwezesha msichana kupata mume

Mwezi Juni umeanza vizuri kwa wateja mbalimbali wa rununu za Samsung ambapo hivi leo Galaxy Tab 8.0 (2019) imepelekewa masasisho ya Android 11 sambamba na toleo namba 3.1 la muonekano wa sura ya mbele (UI 3.1).

Galaxy Tab A

Android 11 yafika kwenye Samsung Galaxy 8.0 (2019).

Katika toleo hilo la Android 11 kwenye simu janja husika pia inakuja na maboresho ya ufanisi wa kufanya kazi, muonekano wa programu tumishi pamoja na masasiho ya kiulinzi yale ya mwezi Mei ya mwaka huu ambayo ni maarufu kutokana na tatizo lililokuwa limeikumba vipuri mama vya Qualcomm.

SOMA PIA  Google Inaweza Ikabadilisha Muonekano Wake Katika Simu Janja!

Katika kufanikisha kuwa simu janja inahama kutoka toleo moja la programu endeshi hadi nyingine ni vyema kuhakikisha kuwa simu janja ina chaji kiasi cha 50% na zaidi lakini pia kifurushi cha intaneti kinachozidi GB 1.3.

Sisi tumefanya kazi yetu ya kukuhabarisha sasa kilichobaki ni wewe kuchukua maamuzi. Daima tunasema usisite kutufuatilia kila siku kwa habari mbalimbali za teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania