Kama una picha, miziki, video na mambo mengine mengi tuu yakiwa yamehifadhiwa katika kompyuta yako ni lazima utakuwa unatumia ma ‘Folder’ mbalimbali ili kuyapangilia mambo yako yote hayo.
Na hii ni kama katika dunia ya kawaida tuu watu wengi huwa wanatumia mafaili maalumu kupangilia nyaraka zao mbalimbali.
Sasa kama ukiwa unapata mafaili mengi kwa wakati mmoja, inakubidi utengeneze ma’Folder’ katika kompyuta yako. Na ukifanya hivyo unaondoka katika kuyapangilia mpaka kwenye kukuchosha, maana yanakuwa mengi sana.
Sidhani kama kuna mtumiaji wa kompyuta yeyote ambaye atapenda kutafuta kwa muda mrefu ili apate faili lake ambalo alilihifadhi ndani ya ‘Folder’ husika.
Ili kuepukana na jambo hili basi kama wewe ni mtumiaji wa Windows ni lazima ujue maujanja haya juu ya ma ‘Folder’ katika kompyuta yako.
- Tengeneza Njia Fupi Za Kufika Kwenye Folder husila
Kama unajikuta mara kwa mara unafungua Folder hilo hilo moja basi haina budi kulitengenezea ‘shortcut’ katika uwanja wa nymbani (desktop). Folder unalolifungua mara kwa mara linaweza likawa ni ‘My Documents’. Sasa ili kuzuia kupitia njia zile zile ile kulifikia unaweza ukalitengenezea njia fupi ya kulifikia (shortcut).
Ili kufanya hivyo nenda katika ‘Folder’ hilo na kabla hujalifungua ‘Right Click’ na kisha chagua ‘Creat A Shortcut’. Lakini kama uko vizuri katika ‘Keyboard’ unaweza ukafuata njia hii ambayo ni rahisi zaidi yaani nenda katika ‘Folder’ unalolitaka kabla hujalifungua ‘Right Click’ na kisha chagua ‘Properties’ na kisha nenda katika ‘Shortcut’. Click ‘Shortcut Key’ na kisha bofya Ctrl katika keyboard utaona “Ctrl+Alt+” ambapo kwa mbele ya jumlisha unaweza ukaongeza herufi yeyote, kwa mfano naweza nikaweka “Ctrl+Alt+D” ili kufungua ‘Folder’ nnalolitaka.
- Jua Machaguo Yaliyofichwa Nje Ya Folder
Kama uko vizuri katika kupangilia ma ‘Folder’ yako basi unaweza ukawa una hamu ya kujaribu njia za aina yake ambazo hazipo katika hali ya kawaida ili kupangilia mambo yako katika kompyuta. Unaweza shangaa hili ni baadhi ya jambo ambalo watu wengi tuu hawalijui.
Jaribu hivi: nenda katika ‘Folder’ lolote, kabla hujaingia ndani yake ukiwa juu yake ‘Right Click’ kwa pamoja ukiwa umeshikilia kibonyezo cha ‘Shift’. Utashangaa kuona machague yameongezeka kama vile Pin to Quick access, Move to Dropbox (kama una Dropbox katika kompyuta yako) au hata Open as Notebook in OneNote.
- Tumia Folder La GodMode
Hivi katika matumizi yako ya kompyuta ulishawahi sikia kitu kinaitwa GodMode?. Kama hukijui ni kwamba GodMode inaweka karibia kila kitu ambacho kipo katika ‘Control Panel’ na kukiweka sehemu moja
Yaani baada ya vitu kuwa vimevurugika katika ‘Control Panel’ ambapo mtumiaji wa kompyuta angelezimika kutafuta baadhi ya vitu. GodMode inaviweka vitu vyote hivyo katika eneo moja ambapo mtu ataweza kuviona na kutumia kwa urahisi.
Ili kuwa na GodMode katika kompyuta yako inakubidi ufanye kama unatengeneza ‘Folder’ Mpya. Yaani ukiwa katika desktop ‘Right Click’ na kisha chagua ‘New’ kisha ‘New Folder’ ukishafika hapo lipo ‘Folder’ hilo jina la: GodMode.{ED7BA470-8E54-465E-825C-99712043E01C} andika hii bila kukosea (kwa usahihi unaweza inakili kama ilivyo) na kisha ukisha bofya kitufe cha ‘Enter’ tuu, Folder la GodMode litatokea.Baada ya hapo ukilifungua utakutana na list kubwa ya mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yangepatikana katika ‘Control Panel’