fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Maujanja

Mfanyakazi: Usiache Kazi Kabla Hujapitia Mtandao Huu!

Mfanyakazi: Usiache Kazi Kabla Hujapitia Mtandao Huu!

Spread the love

Kuacha kazi….Siku ngumu, mbaya au hata ile inayokuacha na mawazo mengi katika kipindi cha kazi inakufanya utamani hata kupigwa ngumi ya uso kuliko mateso unayoyapata moyoni. Mara nyingi siku hiyo itakuacha ukijiuliza maswali mengi, na ni vizuri kujiuliza maswali mengi kama maswali hayo yanahusisha kulipwa kwako (ahah!).

Kabla hujahamaki na kumfuata bosi wako na kumuambia ‘Kazi yako Nakuachia nkah!’ kuna vitu inabidi ujiulize kwanza ili kupata uhakika kwamba uache kazi hiyo au la. Moja kati maswali ya muhimu ya kujiuliza ni kwamba Je, una pesa ya kutosha kujikimua angalau mpaka utakapo pata kazi nyingine au hata ambayo inaweza ikakufikisha miezi sita bila kulipwa?

SOMA PIA  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Maswali mengine yanweza yakawa yale ya ndani kwa ndani kwa mfano Je, ujuzi wako unahitajika sana katika soko la ajira? Maswali yako mengi sana na kabla hayajakuchanganya  hivi unaweza ukawa hujui cha kufanya kabisa.

Hapa sasa ndipo mtandao huu unapokuja kufanya kazi,unaitwa ‘Should I Quit My Job?’ (Tafsiri: Je, Niache Kazi?) na kazi yake kubwa ni kukupa akili ya ziada juu ya swali hilo.

Mtandao Wa Kuutembelea Pale Unapohisi Kuacha Kazi

Should I Quit My Job?

Ndani ya mtandao kuna maswali 25 ambayo ni tofauti ambayo itakubidi uyajaze. Kulingana na wewe na kazi yako mlivyo kuna maswali ya kukubaliana nayo na kuna mengine ya kupingana nayo. Ukishamaliza kuyajibu yote mtandao utakupa majibu yako

SOMA PIA  Ujumbe wa Sauti Whatsapp Status - Uwezo mpya unakuja Whatsapp

Majibu hayo yatakuwa katika ushauri wa aina tatu ambayo ni ; stay, go, look for another job before quitting (Tafsiri: Bakia, Ondoka , Tafuta kazi nyingine kwanza kabla ya kuacha kazi).

Utapata jibu moja kati ya hayo, ukishalipata ndipo hapo utaanza kulifanyia kazi. Watu wengi wanapatwa na changamoto za kufanya kazi ambazo hawazipendi. Mbaya zaidi wanashindwa hata kuondoka katika kazi hizo juu ya sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini huwezi jua kama utatumia mtandao huu unaweza ukawa ndio mkombozi wako

SOMA PIA  Sio ndani dakika 7 tu! Unaweza kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika WhatsApp #Maujanja

Ingia Katika Mtandao Wa https://www.sokanu.com/should-i-quit-my-job Na Uanze Kujibu Maswali au kwa haraka bofya hapa… 

Wafanya kazi ntakuwa nimewagusa leo, Kama nimegusa ntonye sehemu ya comment hapo chini. Kwa habari kama hizi tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila Siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania