Ecobank ni benki ya kiafrika inayopatikana katika nchi 33 barani Afrika. Benki hii pia ina ofisi za kuhudumia wateja wake nje ya bara la Afrika ikiwemo nchi ya Uingereza, China na Ufaransa. App ya Ecobank ni programu maalum ya kwenye simu janja inayokuwezesha kupata huduma za kibenki kwa haraka.

Kuna aina nyingi za akaunti zinazopatikana kwenye App ya Ecobank lakini katika makala hii tutajikita zaidi katika Xpress Account. Xpress Account ni rahisi kufungua na unaweza kuitumia kupata huduma zote za kibenki utakazo hitaji. Ili uweze kufungua Xpress Account unatakiwa kuwa na kitambulisho kimojawapo kati ya kitambulisho cha uraia (NIDA), leseni ya udereva na pasipoti ya kusafiria. Pia utatakiwa kujaza baadhi ya taarifa kama majina yako yote matatu na mahali unapoishi, Baada ya hapo akaunti yako itakuwa tayari na unaweza kuanza kuitumia muda huo huo.

Ukiwa na Xpress Account utaweza pia kupata huduma mbalimbali za kadi ya benki ikiwemo huduma ya Virtua Cards. Huduma hii humuwezesha mtumiaji kutengeneza kadi ya benki ya kidigitali kwaajili ya kufanya malipo ya huduma mbalimbali mtandaoni. Ili uweze kutengeneza Virtual Card unatakiwa kuwa na kiasi cha fedha kisichopungua 11,750/= Tsh, na kadi hiyo inakuwa ni ya VISA.

Huduma zingine unazoweza kupata kupitia Xpress Account ni:
- Kununua muda wa maongezi (Mitandao yote)
- Kulipa Bill mbalimbali kama vile bill ya maji na umeme
- Huduma ya Xpress Cash, Huduma hii itakuwezesha kutoa hela kwenye ATM za Ecobank au kwa wakala wa Ecobank.
- Kufanya Miamala mbalimbali ya hela, Kupitia huduma hii utaweza kutuma na kupokea hela katika mitandao yote ya simu na benki mbalimbali.
- Huduma ya Split Payment, Huduma hii itakuwezesha kugawa hela iliyopo kwenye akaunti yako kutokana na matumizi uliyoipangia.
- Huduma ya EcobankPay, Huduma hii itamuwezesha mtumiaji kulipia huduma za kawaida kama chakula, au bidhaa kwa kuscan (QR Code) au kujaza taarifa za mtoa huduma.
App ya Ecobank inapatikana Playstore kwa watumiaji wa Android na Appstore kwa watumiaji wa iOS. Pakua App hiyo hapa.
–>AppStore
No Comment! Be the first one.